Baadhi ya Viongozi wa Muungano wa wadau
wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa wamebeba
mabango katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo
ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Madaktari wa Muungano wa wadau
wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa katika
matembezi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya
Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na
Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha
na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina,akizungumza na
baadhi ya akina mama wenye watoto wenye ulemavu wa mguu Kifundo katika
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo
sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James
Kiologwe ,akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto
mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa
yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James
Kiologwe,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Muungano wa wadau
wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Bw.Emmanuel Kowero
katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu
Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini
Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James
Kiologwe,akitoa maelezo kwa Mratibu Miguu Kifundo kanda ya Kaskazini
Bw.Goodluck Pallanayo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto
mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa
yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James
Kiologwe, akikata utepe mara baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto
wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma
Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na
Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha
na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina akiagana na Mganga
Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, baada ya kuzindua Cliniki ya
Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa
Mkoa wa Dodoma
Daktari Bingwa Upasuaji Mifupa Hospitali
ya Bugando akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo
sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Picha na Alex Mathias-Wazohuru blog
……………………………..
Na.Alex Mathias,Dodoma
Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa Mkoa,
Dodoma Dkt.James Kiologwe amewaomba wazazi /walezi pamoja na wananchi
kutowafungia ndani watoto wenye matatizo ya mguu kifundo.
Watanzania wameungana na mataifa mengine
Duniani katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mtoto mwenye matatizo
ya Mguu Kifundo ambapo zaidi ya watoto elfu mbili mia tano nchi nzima
hugundulika kuwa na tatizo la ulemavu wa mguu kifundo kila mwaka hapa
nchini.
Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo yaliyofanyika kitaifa
jijini Dodoma Sambamba na Ufunguzi wa Cliniki ya kutibu Dkt.Kiologwe
amesema kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kuwaficha na
kuwanyanyapaa watoto wenye Ulemavu huo.
Aidha amewapongeza wakina mama
walioitikia wito na kupeleka watoto wao wenye changamoto ya mguu
kifundo, pamoja na wadau waliodhamini maadhimisho hayo ikiwemo TCCO kwa
kuchagua mkoa wa Dodoma kama sehemu yakwanza kuadhimisha maadhimisho ya
watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo.
Pamoja na hayo amepongeza taasisi
mbalimbali kwa kushirikiana na TCCO, kwani wamesaidia kuwaondolea adha
watoto pamoja na vijana ambao walikuwa wanaishi kwenye mazingira ya
unyanyapaa lakini wafadhili kwa kushirikiana na TCCO pamoja na wadau
mbalimbali wamerejesha heshima ya utu wa mwanadamu.
Ameongeza kuwa TCCO imeshahudumia watu
zaidi ya elf nne, ambao wamefanyiwa marekebisho ambapo ni watanzania
wengi wamerejeshewa heshima yao ya utu pamoja na mwonekano.
“ Pongezi nyingi ni kwaajili ya nia
iliyomo mioyoni mwetu lakini nilikuwa nawaambia watu kazi ya utabibu ni
zaidi ya kazi ya uaskofu na nizaidi ya kazi ya upadre sisi tunamwangalia
mtu kwa ujumla wake” amesema Dkt. Kiologwe
Pia Dkt. Kiologwe ameeleza kuwa thamana
waliopewa matatibu ni kubwa kwani kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwa
mwanadamu Daktari pekee ndiyo mwenye kutekeleza shughuli zote hizo hata
pale inapohitajika kumrekebisha madaktari hufanya hivyo pia
wanawashukuru wote waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo.
Aidha amesema kuwa TCCO wanajumla ya
matawi 35 kote nchini (kliniki), ambapo Dkt. Kiologwe ameomba taasisi
hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kuanzisha kliniki kwenye kila
mkoa na wilaya kwani takribani katika kila watoto elf moja wanaozaliwa
mtoto mmoja anazaliwa na mguu kifundo.
Awali akizungumza amesema kuwa changamoto
ya ufanisi imekuwa tatizo kubwa sana kwa watoto wenye ulemavu wa mguu
kifundo hasa kwenye utendaji wa kazi, elimu, kushiriki kwenye masuala ya
uchumi pia adha ya kuishi kwenye jamii.
Ambapo ni wastani wa watoto 120, kwa
mwaka wanazaliwa kwenye mkoa wa Dodoma peke yake wakiwa na ulemavu wa
mguu kifundo ikiwa ni pamoja na kukumbana na adha ya kwenda kwenye
matibabu ambapo watu wengi wamezoea masuala yote yanayohitaji
marekebisho yanafanyika kwenye hospitali ya CCBRT, ambayo pia ni msaada
mkubwa katika nchi kwani elimu kuhusu wapi matibabu ya ulemavu wa mguu
kifundo yanapatikana hivyo elimu yakutosha inatakiwa kutolewa kwa umma
ili kujua ni wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana.
Pia ameeleza changamoto ambazo
zinapelekea watu kushindwa kupata matibabu hayo ni pamoja na kipato,
ambapo kwa uzinduzi wa kliniki hiyo ya marekebisho ya mguu kifundo
yatakuwa yanafanyika kila alhamisi na kwa watoto wote chini ya umri wa
miaka mitano matibabu yatakuwa bure.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa
Wadau wanaojihusisha na Matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert
Mhina amesema kuwa bado kuna changamoto miongoni mwa jamii wakihusisha
ugonjwa huo na imani za kishirikina ambapo amesema wanaendelea kutoa
Elimu kwa jamii ili iache kuwanyanyapaa watoto wenye matatizo ya Mguu
Kifundo.
”Rai yangu kwa wazazi/walezi pamoja na
wananchi kiujumla waache kuwafungia na kuwaficha watoto wenye ulemavu
kwani tatizo hilo linaponyeka hivyo jamii iache tabia ya kuwanyanyapaa
pamoja na kuhusisha ugonjwa huu kwa imani za kishirikina”amesema
Dkt.Mhina
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi
ya Wazazi wenye watoto wenye matatizo ya mguu Kifundo wamesema kuwa
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa miongoni mwa
jamii hivyo wameiomba Serikali kufanya msko na kuwachukulia hatua
baadhi ya wazazi wanaowaficha watoto wenye matatizo hayo ya Ulemavu
0 comments:
Post a Comment