Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto), Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Arusha Miundombinu Mahmoud Mansour (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TANFOAM Riaz Lemtula (katikati) na Mshauri wa TANFOAM Victor Njau wakijadiliana na namna ya kumega eneo kwa ajili ya wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha wakati Waziri wa Ardhi alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya kijiji hicho na Mwekezaji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuviu akijadiliana na wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya kijiji hicho na mwekezaji wa Shamba TANFOAM. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lengiroliti na Naaralami wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba TANFOAM NA na SLUIS. Kulia ni Mkurugenzi wa TANFOAM Riaz Lemtula (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir
Shemweta, WANNM MONDULI
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza mgogoro
uliodumukwa muda mrefu baina ya wananchi wa vijiji vya Lengiloriti na Naalarami
vilivyopo wilayani Monduli mkoani Arusha na wawekezaji wa mashamba
yanayomilikiwa na TANFOAM na SLUIS kwa kuamua kumega sehemu za mashamba na
kuwapatia wananchi wa vijiji hivyo.
Lukuvi
alifikia umauzi huo baada ya kukutana na pande zote mbili jana tarehe 23 Aprili
2019 wilayani humo na kujadiliana kwa kina kwa takriban saa tano kwa lengo la
kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umeleta sintofahamu kati ya wananchi wa
vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba.
Katika
makubaliano hayo iliamuliwa ekari kati ya 850 hadi 900 zimegwe kutoka kwa
muwekezaji TANFOAM na kugawiwa kwa kijiji cha Lengiloriti wilayani
Monduli kutoka shamba namba 44 lenye ukubwa wa ekari
3098. Aidha, upande wa muwekezaji SLUIS jumla ya ekari 2000 za muwekezaji
zimetolewa kwa kijiji cha Naaralami, NAFCO, Lokisari na Tukusi ambapo sasa
muwekezaji atabaki na aekari 2217 badala ya 4,217 alizokuwa nazo awali.
Kwa
mujibu wa Lukuvi, ardhi iliyomegwa na kurudishwa katika vijiji hivyo itakuwa
chini ya mamlaka ya kijiji ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la kuigawa upya
kwa wananchi wa vijiji husika na baadaye kupangwa matumizi bora ya ardhi.
Akizungumzia
kijiji cha Lengiloriti, Waziri wa Ardhi aliwataka wananchi wenye Maboma
yaliyokuwa ndani ya eneo la shamba la muwekezaji TANFOAM kuhamia eneo jipya
walilotengewa katika kipindi cha miezi mitatu ili kupisha muwekezaji kuendelea
na shughuli za kilimo na kutotekelezwa kwa aina yoyote agizo hilo kutaifanya
serikali kuchukua hatua.
Maboma
yaliyohamishwa ni pamoja na linaloongozwa na mwenyekiti wa kijiji cha
Lengiloriti Baraka Lemai. Maboma mengine ni la Kaay Rao, Remi Paraleti, Kelemo
Kipara, Yamat Miriliali, Bete Kabulua, Barik Simon, Rais Ramadhani, Ramadhani
Hamis na Lakalai Olodo ambapo Waziri wa Ardhi alisisitiza wamiliki
wa Maboma hayo kupewa kipaumbele wakati wa kugawiwa ekari zilizotolewa na kiasi
kitakachobaki wapatiwe wananchi wengine.
Aidha,
ameagiza kuanzia wiki hii timu ya upimaji ardhi mkoani Arusha iende ktika eneo
hilo kwa ajili ya kuweka mipaka/alama za kudumu ili kuepuka uvamizi
mwingine unaoweza kutokea na kuagiza wawekezaji na wananchi wa vijiji
vilivyopatiwa ekari hizo kuchangia fedha kwa ajili ya upimaji ambapo muwekezaji
na wananchi walikubali kutoa milioni tano kwa ajili ya upimaji.
Kuhusu
mgogoro wa muwekezaji SLUIS, Lukuvi alisema muwekezaji huyo
amekubali kutoa ekari 520 kwa kijiji cha Naaralami pamoja na ekari
300 kwa ajili ya kupitishia mifugo ya wananchi wa kijiji hicho huku ekari 513
zikitolewa kwa NAFCO, 366 kwa Lokisari na ekari 301 kwa kijiji cha Tukusi.
Lukuvi
alisema serikali inawaeshimu sana wawekezaji wa sekta ya ardhi kwa kuwa
wanalipa kodi inayosadia utoaji wa huduma za jamii huku wananchi nao wakipata
ajira na kusisisitiza kuwa wawekezaji wanaomiliki mashamba kisheria serikali
itawalinda na kuonya baadhi ya viongozi wa vijiji kujigawia maeneo bila ya
kushirikisha wananchi wa vijiji husika.
‘’Nimekuja
kusuluhisha mgogoro siyo kunyanganya wawekezaji mashamba, wawekezaji wamekubali
kupunguza mashamba yao na hayo mashamba siyo mali ya wananchi wanaoishi katika
maboma yaliyohamishwa bali ni mali ya kijiji ambacho kitakuwa na jukumu la
kugawa maeneo hayo’’ alisema Lukuvi
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa, baada ya
makubaliano ya pande zote mbili anategemea kila upande utaheshimu maamuzi yaliyotolewa
na mtu yoyote atakayekiuka basi serikali ya mkoa itachukua hatua kali dhidi
yake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanfoam Riaz Lemtula amepongeza jitihada iliyofanywa na Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mpaka kufikia muafaka wa
suala hilo na kuahidi kutekeleza makubaliano waliyoafikiana kwa lengo la kuleta
maendeleo.
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai alimshukuru Waziri wa Ardhi
kwa niaba ya Kijiji chake kwa kazi anayoifanya ya kutatua migogoro ya ardhi na
kuahidi kushirikiana na wawekezaji waiokubali kumega maeneo yao kwa ajili ya
kijiji.
Wawekezaji
wanaomili mashamba katika vijiji hivyo wamekuwa wakiendesha mashamba yao katika
shughuli za kilimo ambapo hulima mazoa ya Maharage, Mtama, Ngwara na mahindi na
kusafirisha mazo hao katika nchi za Sweden, Canada na Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment