METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 21, 2019

WAZIRI WA KILIMO AITAKA TUME YA UMWAGILIAJI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume ya Umwagiliaji jana tarehe 22 Machi 2019 kwenye ukumbi wa Kilimo I Jijini Dar es salaam. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Watumishi wa Tume ya Umwagiliaji wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume ya Umwagiliaji jana tarehe 22 Machi 2019 kwenye ukumbi wa Kilimo I Jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha watumishi wa Tume ya Umwagiliaji jana tarehe 22 Machi 2019 kwenye ukumbi wa Kilimo I, Jijini Dar es salaam. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume ya Umwagiliaji jana tarehe 22 Machi 2019 kwenye ukumbi wa Kilimo I Jijini Dar es salaam.

Na Mathias Canal, Waziri wa Kilimo-Mtwara

Rasilimali maji ni muhimu katika jamii na kama itawekwa vizuri matumizi yake katika kila hatua huleta manufaa makubwa kwa kilimo  kupitia umwagiliaji  na kupata nishati ya umeme kwenye maporomoko.
Mzunguko wa maji, pia unaitwa mzunguko wa Hydrologic yaani mzunguko unaohusisha mzunguko unaoendelea wa maji katika mfumo wa dunia-anga. Kati ya michakato mingi inayohusika katika mzunguko wa maji, muhimu zaidi ni  kugeuza maji kuwa hewa (evaporation), kupumua kwa kuwa maji tena ( condensation and  precipitation)  na mtiririkowake kwenye vijito, mito na maziwa (runoff).
Katika mpango kabambe wa Tanzania wa kufanya kilimo cha umwagiliaji kuwa kipaombele kikuu yaani ASDP II kauli ya kuwa kilimo ni maji inajipambanua zaidi katika kwani inazingatia matumizi bora ya ardhi na maji.
Ili kufikia malengo ya Wizara kuchangamanisha Kilimo na uchumi wa viwanda Waziri wa Kilimo anakemea ufanyaji kazi wa mazoea unaofanywa Tume ya Umwagiliaji kwa kuwa na miradi mingi isiyokamilika.
Waziri Hasunga wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume hiyo jana tarehe 22 Machi 2019 kwenye ukumbi wa Kilimo I Jijini Dar es salaam amewataka watumishi wote kushirikiana na kufanya kazi kwa weledi ili kilimo kiwakomboe wakulima nchini kupitia sekta maalumu ya umwagiliaji.
Alisema malengo ya kilimo hicho cha umwagiliaji ni kuwezesha ufanyaji wa kilimo biashara, Kilimo samaki  na uvuvi na kilimo kwenye maeneo kame kutokana na mabadiliko ya hali ya nchi.
Tanzania jna mabonde tisa (basins) na juhudi za kilimo zimeelekezwa huko kwenye Mabonde ili kumwagilia maji.
Kwenye matumizi ya maji sadifu na kwa gharama nafuu ni mifano ya kule India na Misri ambao wanalima kwenye mabonde yote na jangwani na la maana zaidi ni kuwa India maji yake hutumika mara 6 kabla ya kuishia baharini.
Alisema Tanzania mito mingi hupeleka maji yake baharini  bila kuwa na matumizi rejea na hivyo  kuonekana kuna uhaba wa maji na tathimini iloyofanyika imeonesha kuwa asilimia tano tu ya kilimo chake kiko kwenye umwagiliaji maji huku nchi imebaraikiwa kwa maji ya maziwa makuu matatu na mito mingi kama michirizi ya damu.
Mhe Hasunga alisema kuwa Wizara ya Kilimo sasa imejipanga vizuri katika suala zima la kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija ya kuongeza kiasi cha mazao yatakayozalishwa kwa uwingi na ubora wake na hivyo kutoa faida kubwa na kuoondoa umasikini usio wa lazima nchini kwani ardhi ya kufanya kilimo ipo yakutosha.
“Nitashangaa sana kama sisi wizara tutakuwa tumejipanga kwa ajili ya kuendeleza kilimo kupitia sekta ya umwagiliaji halafu kuna watu mnatukwamisha, nachukia sana mazoea, nakerwa sana na watu kutofanya kazi kwa weledi hivyo  ni klazima mbadilike” Alisisitiza
MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com