Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Bwana Paulo Tarimo wakati akiwasilisha mada kwenye ukumbi wa mkutano wa Misitu uliopo Kihonda Morogoro jana 11.03.2019
Wataalamu
kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali
wamekutana katika Ukimbi wa Misitu uliopo Kihonda Mkoani Morogoro lengo likiwa
ni kujadili Sheria ya kusimamia eneo litakalotengwa kwa ajili ya shughuli za Kilimo ambayo inatarajiwa kuimarisha sekta hiyo
kwa kuleta tija kubwa kwa wakulima na
kuongeza uwekezaji.
Akiongea
katika Mkutano huo wa siku mbili mgeni Rasmi katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe amewashauri wataalamu hao kuhakikisha rasimu
ya Sheria hiyo haingiliani na Sheria nyingine zinazosimamia ardhi.
Aidha
migogoro mingi baina ya wakulima imekuwa ikisababishwa na ukosefu wa Sheria
ya kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya Kilimo hivyo kila Mtu kufanya anavyotaka
alisistiza Mkuu wa mkoa.
Hata
hivyo katika kikao hicho ambacho kimetumika
kuchukua maoni ya wadau Dkt Kebwe amesema
uwepo wa Sheria ya usimamizi wa ardhi ya Kilimo ni muhimu katika usimamizi na uendelezaji wa sekta hiyo hasa kwa wakati huu nchi inapoingia
katika uchumi wa Viwanda.
"Moja
ya changamoto ninazozipata kwenye ofisi yangu ni kuitambua ardhi ya Kilimo, wanakuja
wawekezaji kwenye kilimo lakini kukosekana
kwa sheria kama hii inayoonesha ardhi ya kilimo Kwa ajili ya matumizi ya wananchi na wawekezaji inakuwa ni changamoto
kubwa." alisema Mkuu Wa mkoa Dkt Kebwe Stephen .
Alisema
mipango inayoendelea kutekelezwa na serikali kupitia wizara ya Kilimo inaonesha
nchi inaweza kulisha mataifa mengine ya Afrika na nje ya bara hili ambapo Sera
na Sheria zitatumika kuimarisha Kilimo na kuwalinda wakulima wetu alisisitiza Mheshimiwa
mkuu Wa mkoa.
Naye Mkurungezi
wa kinalindaMipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Bw Paulo Tarimo amesema
mchakato wa kuandaa Sheria ya Kilimo ni muhimu kwa kuwa utasaidia kuitambua ardhi
ya Kilimo ki Sheria pamoja na Sheria.
Akiwasilisha
mada yake Mkurugenzi huyo amesema hakuna kipengele ambacho kinalinda ardhi ya Kilimo
hivyo Sheria hii ni muhimu kwa sababu pamoja na kusimamia matumizi bora ya ardhi
lakini itasaidia mipango mbalimbali ya kalimo.
Gungu
Mibavu Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipago akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo
amesema wazo La kuwa na Sheria ya usimamizi wa ardhiya Kilimo lilianza toka 2009 ambapo michakato
mbalimbali imeendelea ili kupata Sheria hiyo.
Aidha
Sheria hiyo itasimamia shughuli zote za ugani ardhi ya Kilimo na taratibu zote
za zana za kilimo
Awali
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania MVIWATA Bwana
Stepen Ruvuga amesema kwamba sheria hii inatakiwa kuwa na maslahi mapana kwa
wakulima kwa kuwa Kilimo pamoja na kwmba ni kichocheo cha maendeleo lakini pia ni
uhai wa wakulima wadogo.
Hata
hivyo Bwana Stephen Ruvuga amesema Sera nyingi pamoja na baadhi ya Sheria
zimeandaliwa pasipo kumshirikisha
mkulima mdogo na kuangalia mahitaji yake lakini zimekuwa zikijali maslahi ya wakulima
wakubwa na wawekezaji hivyo Sheria hii inaweza kuwa na tija kwa sababu imekuwa shirikishi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment