Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akikagua shamba la mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza, Jana machi 11, 2019.
Sehemu ya washiriki wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria) uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania Bw H.E Antonio akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria) uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza, Kulia kwake ni naibu Waziri wa kilimo mhe Innocent bashungwa.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo
Tanzania na Brazil zimeingia
makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.
Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika
hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta
hiyo ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.
Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil
nchini Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini
wanapata Pamba mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze
kuongeza tija.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema
hayo jana tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya
mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.
Mhe Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania
inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja
kuimarisha sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha
inazalisha mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote
nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba
manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko
Pamba Manyonya.
Alisema Wizara ya kilimo itakuwa na
jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi
pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema
maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam
waka 2015-2020.
Aidha, alisema kuwa Serikali pia imejipanga kupanua
maabara za utafiti wa zao la Pamba ili kuimarisha ufanisi na tija ya zao hilo
kwani mafanikio ya kilimo yanategemea zaidi katika utafiti.
Mhe Bashungwa ameishukuru
serikali ya Brazil kwa utekelezaji wa mradi huo nchini Tanzania ambao unatokana
na mahusiano mazuri katika nchi hizo mbili inayoakisi katika kufungamanisha kilimo
na uchumi wa viwanda.
Kadhalika alisema serikali
tayari imeanzisha vituo viwili vya kuzalisha Pamba mbegu vipara katika mkoa wa
Simiyu pamoja na Mkoa wa Tabora
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment