Na Francis Daudi, Bangalore!
+919513833624.
Katika ulimwengu huu tunaoishi kuna baadhi ya watu hujitokeza kuwa mifano muhimu kwetu, labda kwa jinsi walivyoweza kutumia fursa walizopata kwa ufanisi kuweza kufanikiwa zaidi.
Mwezi Mei mwaka huu Mgombea wa vuguvugu la En Marche! Bwana Emmanuel Macron alishinda uchaguzi mkuu nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 39 tu! Hii ni historia mpya katika bara la Ulaya na dunia. Alimwangusha Bi Marine Le Pen wa chama cha The National Front (FN).
Lakini nyuma ya ushindi huo alikuwepo kijana mdogo zaidi bwana Ismael Emelien, Yeye aliongoza timu ya ushindi na vuguvugu la En Marche! Lililompeleka ikulu raisi mteule Emmanuel Macron. Kiufupi Emelien, sio mtu anayejulikana sana, Lakini ndiye alipewa jukumu zito kabisa kama Mshauri mkuu wa Mgombea wakati wote wa kampeni.
Miezi 13 kabla ya uchaguzi, Emelien aliandaa mpango kazi ambao ulipaswa kutekelezwa! Alimshauri Macron aina ya watu wanaohitajika katika timu ya kampeni. Macron alimwamini na kutekeleza.
Haikuwa rahisi kwake, kwani ilimpasa kuandaa mbinu na mambo mapya ambayo yangeweza kuwavutia wapiga kura ambao wanaelewa vizuri siasa za kisasa.
Aliacha kazi katika Wizara ya Fedha na Masuala ya Uchumi kisha kwenda kuanzisha vuguvugu la En Marche!. Ilimpasa kupita mitaani akiwa na washirika wengine kushawishi watu kujiunga nao, aliongoza timu iliyokusanya maoni juu ya mambo mbalimbali kisha kuyachambua na kujenga mtandao mkubwa juu mpaka mitaani ulioitwa "Grande March". Haikuwa timu kubwa yenye uzoefu wa kutosha lakini yenye ari kubwa ya ushindi.
Emelien ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29 tu(Mwisho wa mwaka huu 2017 atafikisha miaka30) alijiingiza katika masuala ya siasa akiwa na miaka 19 alipojitosa katika timu ya Dominique Strauss-Kahn aliyeshindwa katika uchaguzi wa mwaka 2007. Alipoingia katika timu hiyo ya kumsaidia Bwana Strauss-Kahn ilimbidi kuachana na masomo ya chuo kikuu. Hapa Emelien anatufunza kujitoa kwa kile tunachokitaka!
Lakini Bwana Strauss-Kahn alishindwa uchaguzi akiwa na chama chake cha kijamaa. Emelien alijiunga na taasisi ya Jean-Jaurès, kisha akarudia masomo na kuhitimu mwaka 2010. Baadae alijiunga na kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya Havas Group.
Alirudi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa Ufaransa mwaka 2013 akisaidia timu ya Nicolás Maduro. Hapo aliendelea kujifunza mambo mengi, Mpaka wakati huo alishakuwa na urafiki wa karibu na Emmanuel Macron toka mwaka 2009. Vijana wa Uvccm tunauvumilivu mambo yanapokwama? Au tunakimbilia kulaumu?. Emelien anatufunza kuwa wavumilivu na kujipa muda katika kujifunza zaidi.
Hivyo basi Macron akiwa waziri mwenye dhamana katika Wizara ya Fedha na Masuala ya Uchumi alimpendekeza kuwa msaidizi wake wa karibu. Katika kujiandaa kuwa political strategist ilimpasa Emelien kujifunza lugha nyingi(Anaongea lugha tano kwa ufasaha).
Vijana wenzangu wa ccm tunapaswa kujinoa kitaaluma kadiri muda unavyoruhusu. Dunia ya sasa inahitaji watu wanaoweza kuwa na maarifa yanayoweza kutupeleka mbele katika ndoto zetu na taifa letu.
Ismael Emelien anaelezwa kama mtu mtulivu, anayetumia muda wake katika kusoma vitabu(bookworm), na pia ni mtu wa kufanya kazi. WanaUvccm wenzangu siasa za wakati huu zinahitaji stadi nzuri, si wakati wa kuishi kwa mazoea. Tujipe maarifa na ujuzi mpya kupitia vitabu. Wakati akiongoza vuguvugu la "Grande March" akiwa na wabobezi wengine katika mambo ya uchaguzi na kampeni kama Liegey Muller Pons hakuwa analala akizungukia wanaharakati nyakati za usiku.
Emelien ni kama kijana mwingine wa Tanzania tu, Yeye amezaliwa mwaka 1987 katika familia ya kawaida kabisa kwenye eneo la Grenoble. Anatufundisha vijana wa Tanzania na Afrika kufanya kazi kwa bidii; Kujituma na Umri au Mazingira uliyokulia hayawezi kuwa sababu ya kushindwa.
Emelien hakuzaliwa katika familia yenye ‘connections’ ila yeye amepigana mpaka kuonesha uwezo wake. Sio mtu wa majivuno na hajitokezi mara nyingi kwenye vyombo vya habari. Kila nafasi aliyopata ameitumia vizuri na kwa uaminifu mkubwa. Uwezo wake katika kuchambua na kuandaa mikakati umempeleka mbele zaidi.
Jarida maarufu la Ufaransa, lilimtaja kama kijana anayeonekana mara zote akishika simu ya Macron huku akijificha kwa miwani yake kubwa na kutarajiwa kuiongoza Ufaransa kupitia raisi mteule Emmanuel Macron.
Imeandaliwa na Francis Daudi, Bangalore(India)
Mwanahistoria kijana na mchambuzi wa Masuala ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment