Naibu Waziri
wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Omari T. Mgumba (Mb.) (kulia) akiongea na Naibu Mkurugenzi Mkuu kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje ya Israel ambae pia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya MASHAV, Bw. Gil Haskel
walipofanya kikao katika Ofisi ya
Naibu Waziri wa Kilimo, iliyopo Kilimo IV, Mjini Dodoma hivi karimuni.
Na
Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo – Dodoma
Serikali kupeleka
wataalamu 100 wa kilimo nchini Israel ili kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa za kuendeleza
kilimo cha umwagiliaji nchini.
Hayo
yamebainishwa wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba
(Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ambae pia
ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya MASHAV, Bw. Gil Haskel walipofanya kikao katika Ofisi ya Naibu Waziri wa Kilimo,
iliyopo Kilimo IV, Mjini Dodoma
Mhe. Mgumba
amebainisha kuwa, nafasi hizo za masomo
ya kilimo nchini Israel zitatoa fursa kwa wataalam hao kuongeza ufanisi katika
Sekta ya kilimo nchini na kukifanya kilimo kuwa na tija zaidi.
Aidha, Naibu
Waziri wa Kilimo amesema kuwa, tatizo kubwa la Sekta ya Kilimo nchini ni
uzalishaji mdogo usiokuwa na tija ambapo
wakulima hutumia nguvu kubwa lakini matokeo yanakuwa madogo. Hivyo, Naibu
Waziri huyo alisisitiza kuwa, wakulima nchini wanatakiwa kuzingatia mbinu bora
za kilimo, matumizi sahihi ya pembejeo, mbolea na pia kutumia mbegu bora ili
kuweza kumnufaisha mkulima.
Akiongea na mgeni
huyo kutoka Israel, Mhe. Mgumba amebainisha
kuwa, mabadiliko ya tabianchi yanaathiri
kwa kiasi kikubwa Sekta ya Kilimo hivyo
ni muhimu kilimo cha umwagiliaji kikaanza kutumika maeneo mbalimbali ya nchi
kwa sababu ya uwepo wa vyanzo vya maji vya kutosha na sio kuendelea kutegemea
kilimo cha mvua ili kupambana na hali
hiyo.
Pia, Mhe.
Mgumba amesisitiza kuwa, serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekuwa ikihamasisha
wakulima nchini kuanza kufanya kilimo cha kibiashara ili kuweza kuongeza kipato
chao.
Aidha,
ametoa ufafanuzi kwa mgeni huyo kuwa, Serikali
ya Israel bado inaweza kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwekeza
katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa bado eneo linalotumika kwa kilimo hicho
ni dogo ikilinganishwa mahitaji.
“Hadi sasa
eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 475,000 na Mkakati wa
Serikali ni kufikia hekta milioni moja ifikapo mwaka 2035”alisema Naibu Waziri,
Mhe. Mgumba.
Aidha, Mhe.
Mgumba ameiomba Serikali ya Israel kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kuendeleza bonde la mto rufiji kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili wakulima
wengi waachane na kilimo cha kutegemea mvua kama ilivyo sasa.
Awali, Mhe.
Mgumba alimfahamisha Mtendaji Mkuu huyo wa Taasisi ya MASHAV kwamba, bado kuna
fursa ya uwekezaji katika eneo la uhifadhi wa mazao kwa kuwa hali ya upotevu wa mazao baada ya mavuno ni asilimia
40 ikilinganishwa na nchi ya Israel ambayo upotevu ni asilimia 20. Akifunga
Kikao hicho, Mhe. Mgumba alisema kuwa, ili kilimo kiwe na tija na kuweza
kumkomboa mkulima nchini, lazima kuacha kutegemea mvua za msimu pekee na hivyo
kuanza kutumia kilimo cha umwagiliaji nchini.
0 comments:
Post a Comment