Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA Kanda ya Mashariki na kati inayojumuisha mikoa ya Tanzania, Rwanda na Uganda Prof Nuhu Hatibu (Wa Pili Kulia) mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo Jijini Dar es salaam, Wengine ni Meneja wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA nchini Tanzania Ndg Vianey Rweyendela (Kushoto) na Kiongozi wa timu ya uratibu wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo - ASDP II kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Zakaria Muyengi (Kulia) leo tarehe 22 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifanya mazungumzo na Mkuu wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA Kanda ya Mashariki na kati inayojumuisha mikoa ya Tanzania, Rwanda na Uganda Prof Nuhu Hatibu mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo Jijini Dar es salaam, Wengine ni Meneja wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA nchini Tanzania Ndg Vianey Rweyendela na Kiongozi wa timu ya uratibu wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo ASDP II kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Zakaria Muyengi leo tarehe 22 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiagana na Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa wafadhili wa maendeleo upande wa kilimo- Tanzania Ndg Fred Kafeero mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiagana na Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa wafadhili wa maendeleo upande wa kilimo- Tanzania Ndg Fred Kafeero mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenela Mkangalla mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2019
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar
es salaam
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Februari 2019 amekutana na
kufanya mazungumzo na Mkuu wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA Kanda
ya Mashariki na kati inayojumuisha mikoa ya Tanzania, Rwanda na Uganda Prof
Nuhu Hatibu sambamba na Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania ambaye
pia ni Mwenyekiti wa wafadhili wa maendeleo upande wa kilimo- Tanzania Ndg Fred
Kafeero.
Katika
Mkutano huo Waziri Hasunga ameeleza dhamira ya serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imeanza zoezi la kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo
likiwa ni kuwatambua ili kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na
uzalishaji katika mazao yote.
Hasunga alitoa
agizo hilo tarehe 29 Disemba 2018 wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za
Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.
Mhe. Hasunga alisema
ili kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya kilimo na kuandaa mipango
madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua Wakulima wote nchini na
kuongeza kuwa Wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa
kwa Wizara yake kufanya jambo kama hili katika mazao mengine hapa
nchini.
Waziri Hasunga aliongeza
kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza Wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe
hadi kufikia katika hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa
na mfumo maalumu wa kanzi data (Database) ya kuwafahamu ili kushughulikia
mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.
Vilevile ameeleza umuhimu wa
kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto
zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla. “Kuna kila
sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya
Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia
inahitaji kupitiwa upya” Alisema
Alisitiza pia
kuwa serikali imedhamiria kuanzisha Bima ya mazao ya wakulima nchini kwani hiyo ni hatua nzuri katika kuhuisha utoaji
wa huduma bora za bima za kilimo kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Bima ya
Mwaka 2009, Sheria na Mipango Mbalimbali katika sekta ya kilimo; kwa kutafutia
ufumbuzi wa pamoja changamoto zinazokabili sekta ya kilimo na wakulima nchini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika-AGRA Kanda ya
Mashariki na kati inayojumuisha mikoa ya Tanzania, Rwanda na Uganda Prof Nuhu Hatibu
amempongeza waziri wa kilimo huku akisisitiza kuwa AGRA inaunga mkono zoezi la
usajili wa wakulima na ipo tayari kushirikiana na serikali katika zoezi hilo.
Naye,
Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa
wafadhili wa maendeleo upande wa kilimo- Tanzania Ndg Fred Kafeero amesema kuwa
shirika hilo litaendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuiinua sekta
ya kilimo nchini.
Katika hatua nyingine Mhe Hasunga amekutana na kufanya
mazungumzo na aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenela Mkandalla.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment