Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Katikati) akiongoza kikao kazi cha Wabunge wa maeneo yanayolima pamba nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini, Dodoma leo Jumatatu tarehe 4 Februari, 2019. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) na Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumbwa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Pichani kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe Willium Ngeleja, Mhe. Kiswaga Boniventura Mbunge wa Magu, na Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini, Dodoma leo Jumatatu tarehe 4 Februari, 2019.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri
wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amewaambia Waheshimiwa Wabunge wa maeneo
yanayolima pamba kuwa Wizara ya Kilimo imedhamiria kumkomboa Mkulima wa pamba
na kwa kuanza imeanzisha zoezi la kuwasajili Wakulima wote nchini wakiwemo Wakulima
wa pamba ambapo Serikali imetengeneza mfumo maalumu wa kuwatambua kwanza
Wakulima, maeneo wanayotoka, mashamba yao yapo wapi na yana ukubwa gani.
Mhe.
Hasunga ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu na Waheshimiwa Wabunge hao
katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini, Dodoma leo Jumatatu tarehe 4
Februari, 2019.
Kikao
hicho kilikuwa na lengo la kufanya maboresho kwa ajili ya kujiandaa na msimu
ujao wa mauzo ya pamba ambao unatarajia kuanza Mwezi Aprili mwaka huu.
Mhe.
Hasunga amesema moja ya mambo ambayo Wizara ya Kilimo itahakikisha inayashughulikia
ipasavyo, sambamba na kuwatambua Wakulima wa pamba ni pamoja na kuupitia upya
mfumo wa Ushirika katika ununuzi wa pamba, mfumo wa uagizaji na uingizaji wa
viuatilifu vya pamba pamoja na masoko ya zao hilo.
Waziri
Hasunga amesema katika kipindi hiki kifupi amekuwa akipata malalamiko mengi kutoka
kwa Wakulima wa mazao mbalimbali kuhusu udhaifu wa mfumo wa uagizaji wa
uingizaji wa pembejeo za kilimo yakiwemo madawa na mbegu hafifu.
“Napenda
nikiri kuwa tuna tatizo katika mfumo wa uagizaji na uingizaji wa pembejeo za
kilimo, bado haujakaa vizuri lakini baya zaidi ni viuatilifu hafifu. Serikali
kamwe haiwezi kutazama Wakulima wakionewa na Wajanja wachache na huu ni uhujumu
uchumi lazima wanaofanya mambo haya wachukuliwe hatua kali za kisheria”.
Amekaririwa Waziri Hasunga.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya Wabunge wameshauri kuwa muda wa kupeleka pembejeo
za kilimo kama mbegu bora na madawa uwe mapema zaidi kuliko ilivyo sasa. Mhe. Kiswaga
Boniventura Mbunge wa Magu ameishauri Serikali kuwa wakati wa zoezi la ununuzi
wa pamba ghafi zoezi hilo liendane na zoezi la kuwapelekea Wakulima mbegu bora
za pamba na kuongeza kuwa litaokoa fedha za Umma kwa kuwa fedha za usafirishaji
itatumika mara moja tu.
Naye
Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga amesema kuna haja kubwa ya kupitia mfumo
mzima wa Vyama vya Ushirika vinavyonunua pamba, akitoa mfano katika msimu wa
pamba uliopita wa mwaka 2018/2019 Wakulima wa pamba walikuwa wakikatwa shilingi
100 katika kila kilo moja kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa viuatilifu (Madawa
ya pamba) katika msimu ujao wa kilimo.
Mhe.
Njalu amesema kuna maeneo mengi ambayo Wakulima wengi wanafikisha zaidi ya kilo
mia tano (500) na anapokatwa kiasi hicho cha fedha makusanyo yanakuwa makubwa
hadi kufikia shilingi elfu hamsini (50,000/=) wakati thamani halisi ya pembejeo
ambazo atapewa na Chama chake cha Ushirika hakizidi shilingi elfu kumi
(10,000/=).
Mhe.
Waziri Hasunga amekiri kuwa jambo hilo linaweza kuwepo na kuna haja ya kuufanya
maboresho makubwa mfumo mzima ununuzi wa pamba kabla ya kuanza msimu mpya wa
ununuzi wa pamba ambao unataraji kuanza mapema Mwezi Aprili, 2019.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment