METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 22, 2019

TADB YAJA KIMKAKATI KUZUIA UPOTEVU WA MAHINDI BAADA YA KUVUNA

Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza na wasindikaji na wadau zao la mahindi wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Dar es Salaam
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa wito kwa wakulima na wasindikaji wa zao la mahindi kuwekeza katika teknolojia za kisasa kwa lengo la kuzuia upotevu wa mahindi baada ya kuvunwa ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha wakati akizungumza na wawekezaji katika usindikaji wa zao la mahindi mara baada ya kuzindua mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo.
“Natoa wito kwa wasindikaji kutumia fursa za mradi huu ili kuongea tija katika shughuli zao,” amesema.
Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando amesema kuwa mfuko huo umelenga kuwajengea uwezo wasindikaji wa ndao kuwa sehemu ya uongezaji wa thamani wa mnyororo wa zao hilo.
“Tunaamini Mradi huu utasaidia kuzuia upotevu wa mahindi hivyo kuleta tija kwa wakulima wa zao hili,” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya wasindikai walioshiriki katika uzinduzi wa Mradi huo, Bw. Savior Chanay kutoka Kampuni ya Real World ya mkoani Ruvuma ameishukuru Serikali kupitia TADB kwa kuja na Mradi huo ambao utaongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mahindi.

“Mradi huu utaleta tija katika shughuli zetu za kila siku hivyo kuongeza uwezekano wa kuongeza kipato kwa wakulima wa mahindi,” amesema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com