Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisiitiza jambo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri akitoa taarifa ya Mkoa huo mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kabla ya kufungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019.
Mzee Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa maelezo ya awali kuhusu Tumbaku wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019.
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Shinyanga (KACU) na baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora
Bodi
ya Tumbaku nchini imeagizwa kuhakikisha kuwa Wakulima wote wa zao hilo wanasajiliwa
katika mfumo unaoeleweka kwani hilo ni lengo la haraka la Wizara kwa taasisi
zote la kuwasajili wakulima wote nchini ili kujua kiasi cha maeneo wanayolima.
Hayo yameelezwa leo tarehe 17
Januari 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa
Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mhe
Hasunga ameitaka Bodi ihakikishe kwamba tumbaku yote itakayovunwa msimu huu inauzwa
ifikapo Juni 2019 sambamba na kuagiza masoko kuwahi kuanza msimu huu ili
kurahisisha kuanza mapema maandalizi ya zao hilo msimu wa 2019/2020.
Vilevile
Waziri Hasunga ameagiza upatikanaji wa pembejeo kwa wakati. “Hili linaenda
sambamba na utekelezaji wa Agizo la Mhe:
Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) - Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
la kuhakikisha unakuwepo utaratibu wa kumwezesha mkulima anajitegemea kwa
pembejeo ili aache kuwa tegemezi wa mikopo ya mabenki” Alikaririwa Mhe Hasunga
Mhe
Hasunga alisisitiza kuwa lazima Bodi kutilia mkazo malengo ya muda mrefu kwenye
Tumbaku ambayo ni pamoja na utafutaji
wa masoko (mhakikishe mnapata wanunuzi wengine wapya ifikapo 2022), Kuhakikisha
kuwa kwa ubia au ushirikiano uliopo kijengwe
kiwanda kipya cha kuchakata tumbaku ili kutoa ushindani wa gharama za uchakataji
wa tumbaku nchini, Kuongeza ubora wa zao kutoka asilimia 87 ya sasa hadi asilimia
92 ifikapo June 2022 na Kuongeza mbegu mpya na bora za tumbaku ili kuweza
kupenyeza katika masoko ya nchi zingine kama China n.k.
Tumbaku
ni miongoni mwa mazao makuu matano ya kimkakati ya biashara katika Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe: Dkt.
John Joseph Pombe Magufuli – Rais waJamhuri ya Muunganowa Tanzania. Mazao
hayo ni Tumbaku, Kahawa, Pamba, Korosho,
na Chai. Takwimu zinaonesha kwamba kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2016 tumbaku imekuwa na mchango mkubwa kuliko mazao
mengine makuu ya biashara kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
“Natambua juhudi mnazofanya katika hifadhi ya mazingira.
Lakini mnatakiwa muongeze juhudi kwani taarifa zinaonesha kuwa hadi kufikia msimu
wa kilimo uliopita wa 2017/2018 wastani wa miti iliyopona baada ya kupandwa na
wakulima ni asilimia 40.46 tu,
kiwango hiki hakiridhishi maana kiko chini mno” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema
Ili uzalishaji wa tumbaku uwe katika mtazamo wa kibiashara wataalam mnapaswa kuwaelimisha wakulima ili waelewe kwa dhati umuhimu
wa kuzingatia taratibu za kilimo cha
tumbaku (Compliance).
Alisema kuwa Baadhi ya
wakulima katika vyama vya msingi vya ushirika wameshindwa kulipwa malipo yao
kutokana na vyama kuwa na madeni yasiyokuwa wazi na yasiyolipika. Hali hii
imesababishwa na ubadhirifu wa baadhi viongozi na watendaji wasio waaminifu
katika ushirika, utoroshaji na ulanguzi wa tumbaku.
Moja ya
maeneo yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala yanayohusu hatua
za kutatua changamoto za kulikomboa zao la tumbaku na kulipa sifa zinazohitajika
katika soko la dunia. Mfano wa masuala hayo ni pamoja na Wingi na ubora wa zao, Kuongeza
tija, Malipo stahili kwa wakulima, Utunzaji wa Mazingira na Kuzuia
utumikishwaji wa watoto.
Kupitia
mkutano huo Waziri wa Kilimo amebainisha kuwa Serikali iko thabiti kusimamia
uendelevu na uzalishaji wenye tija wa zao la tumbaku kama zao mojawapo la
biashara la kimkakati. Ni kwa msingi huo, Serikali inaendelea na jitihada za kupata
ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya tumbaku.
“Tarehe 28-30/12/2018 niliwaita viongozi wa Bodi za
mazao ikiwa ni pamoja na Bodi ya Tumbaku na kuwapa malengo ya muda mfupi (Januari
- Juni, 2019) na mrefu (Julai - Juni, 2022) ni pamoja na nyie wadau katika
nafasi zenu mshirikiane ili kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa” Alisisitiza
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe
Agrey Mwanri alisema kuwa mkutano huo maalumu wa mwaka wa wadau wa Tumbaku ni
mkutano ambao upo kwa mujibu wa sharia ya sekta ya Tumbaku Na 24/2001 kifungu
cha 49 cha marekebisho ya sheria yam waka 2009 ambao imeweka ulazima wa wadau
kukutana walau mara moja kwa mwaka kujadili masuala mbalimbali ya kuendeleza
sekta hii na kutatua changamoto zilizopo na kukubaliana utaratibu wa
ugharamiaji wa majukumu ya pamoja ambayo yameainishwa na sharia ya sekta ya
Tumbaku.
Alisema uwepo wa mkutano huo
umekuwa miongoni mwa mikutano yenye tija kwa kukutanisha madau wote na kuwa na
mikakati ya pamoja, kuongeza ufanisi wa masoko ya Tumbaku, na uhai wa kutunza
mazingira kwa kupanda miti kwa pamoja.
Kwa upande wake Mzee Hassan
Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa taarifa ya utangulizi wakati wa mkutano
huo alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Tumbaku kuwa ni
pamoja na kutokuwepo kwa mkakati utakaotekeleza na shirikishi wa uhifadhi wa mazingira, kuchelewa kwa
upatikanaji wa mikopo ya pembejeo kwa ajili ya kununua pemebejeo za kilimo.
Zingine ni utaratibu wa
upatikanaji wa bei ya zao la Trumbaku katika kuhakikisha kuwa bei inapatikana
mapema na kwa wakati, kushuka kwa mahitaji ya Tumbaku katika soko la Dunia,
Kushuka kwa ubora wa Tumbaku ambao unachangiwa na masuala mbalimbali, Vita
dhidi ya matumizi ya Tumbaku Duniani na kuboreka kwa bei ya pembejeo.
Sambamba na hayo pia ameishukuru
serikali kwa mchango wake kwenye sekta ya Tumbaku kwa ushirikiano inaouonyesha
katika suala la kuhakikisha kuwa wanapatikana wasambazaji wa pembejeo za kilimo
na kufanikiwa kupunguza bei ya pembejeo za kilimo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment