Wananchi
wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha
kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya
kata
Kilio
hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala
Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo
kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano
kuwa magumu.
“Changamoto
nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii
inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za
maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa
mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.
Halikadhalika
jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Mh. Desderius
Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa
mawasiliano hayo yanapatinaka na hatimae kurahisisha utendaji kazi wa shughuli
za maendeleo katika kata hiyo.
“Hawa
wananchi ni pekee ambao hawazungumzi na wenzao katika taifa na katika jimbo,
juhudi nilizozifanya kama kiongozi wa jimbo ni kuitaka wizara ihakikishe kwamba
tunapata mtandao, tunashukuru mungu wametusikiliza na sasa wanajenga minara
miwili katika Kijiji cha kilambo cha mkolechi na Kijiji cha Kala, wanasema Kala
itazungumza wantuambia katika kipindi kisichozidi miezi miwili,” Alibainisha.
Nae Mh.
Wangabo aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwa mawasiliano yataimarishwa
“Tutaimarisha hayo mawasiliano na juzi nilikuwa naongea na waziri wa ujenzi
alikuja pale ofisini na tuliongea swala hili la minara ya mawasiliano, uzuri
wameshaanza kufanyia kazi, kwahiyo tutaongeza nguvu kule ili mitandao ya
mawasiliano ifanye kazi n ahata radio nkasi iweze kuwafikia huku,” Alisema.
0 comments:
Post a Comment