Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Walioketi kushoto ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia kubadilishana nyaraka
baada ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia
Zikankuba na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP)
Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
leo Ijumaa Januari 4, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza wakati wa utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia
Zikankuba na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP)
Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
leo Ijumaa Januari 4, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford
pamoja na Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary
Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa, Viongozi wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama na maafisa wengine waandamizi wa taasisi hizo baad ya
hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwenye
hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019.
Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na
Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford pamoja na
Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu
Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwana maafisa wengine waandamizi wa UNFPA
baada ya hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati
ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani
(WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa
Januari 4, 2019. Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na
Dkt Omary Mgumba. PICHA NA IKULU
Na
Mathias Canal, NFRA-Dar es salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Leo tarehe 4
Januari 2019 ameshuhudia utiaji saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la chakula Duniani
(WFP).
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli
ameipongeza Wizara ya kilimo kwa kuwatafutia masoko wakulima na kuongeza kuwa
inapaswa kuongeza msisitizo wa kutafuta masoko ya Mazao mengine ya wakulima
nchini.
Pamoja
na pongezi hizo za Mhe Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya kilimo kupitia NFRA
na kuiagiza Wizara ya kilimo kushirikiana na Taasisi zingine za serikali
ikiwemo jeshi la Polisi, Wakala wa Barabara (TANROADS), Shirika la viwango
Tanzania (TBS), Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Shirika la reli Tanzania
(TRC), na mamlaka ya usimamizi wa bandari (TPA) kuhakikisha wanaondoa
urasimu na kuharakisha ununuzi wa Mazao yanayonunuliwa na WFP ikiwemo Tani
36,000 za mahindi ili wakulima wanufaike na fursa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu
imeeleza kuwa mkataba huo umetiwa saini na Kaimu Mtendaji Mkuu wa NFRA Bi
Vumilia Zikankuba na Mwakilishi wa Mkurugenzi mkazi wa WFP hapa nchini Bw
Michael Danford ambapo WFP inanunua mahindi yenye thamani ya Shilingi Bilioni
21 kutoka NFRA.
Mhe
Rais Magufuli ameipongeza WFP kwa uamuzi wake wa kununua chakula kutoka
Tanzania kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa nchi zenye matatizo ya chakula na
ameitaka NFRA kutoa Tani zote 45,000 za mahindi ambazo WFP waliomba kununua,
ili fedha hizo zitakazopatikana ziweze kununua mahindi mengine kwa wakulima.
Vilevile
Rais Magufuli ameiagiza NFRA kuuza mahindi kwa WFP hata kama watahitaji mahindi
Tani 100,000 au 200,000 kwani kufanya hivyo kutawarahisishia kwenda sokoni
kununua mahindi mengine jambo ambalo linaimarisha soko la wakulima.
Ameitaka
NFRA kujipanga vizuri ili kujiendesha kwani serikali haitotoa fedha kila mwaka
kwa ajili ya kununua mahindi ya kuhifadhi huku akiwataka wafanyabiashara kuacha
kulalamika badala yake kufanya biashara kwa uwazi na serikali itawaunga mkono.
Awali,
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara ya kilimo
imejipanga kuimarisha soko la wakulima ndani na nje ya nchi hivyo wakulima
hawapaswi kuwa na wasiwasi badala yake wanapaswa kuongeza tija katika
uzalishaji kwani serikali knawatafutia soko.
Bashungwa
alisema kuwa Wizara ya kilimo imechukua hatua kadhaa za kuimarisha mazingira
kwa WFP kunua mahindi na Mazao mengine hapa nchini ambapo jambo hilo
litafanyika sambamba na kufungamanisha uchumi wa Viwanda.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment