METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 4, 2019

Mhe Mgumba aanza ziara ya kikazi Jimboni kwake

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Mgumba ambaye ni naibu waziri wa Kilimo akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya siku sita Jimboni kwake Morogoro Kusini Mashariki iliyoanza Tarehe 01/01/2019.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Mgumba ambaye ni naibu waziri wa Kilimo ameanza ziara ya kikazi ya siku sita Jimboni kwake Morogoro Kusini Mashariki Tangu Tarehe 01/01/2019 Mpaka Tarehe 06/01/2019.
Pichani Mhe Naibu waziri Omary Mgumba watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji na Shule ya Msingi Vuleni baada ya kutembelea Ujenzi wa shule unavyoendelea baada ya Serikali kupeleka fedha zaidi ya Shilingi Milioni Sitini na sita kwa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa kwenye Shule hiyo wakishirikiana na Nguvu za wananchi na ambapo amechangia tofali elfu mbili (2000).
.............................................

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Mgumba ambaye ni naibu waziri wa Kilimo ameanza ziara ya kikazi ya siku sita Jimboni kwake Morogoro Kusini Mashariki Tangu Tarehe 01/01/2019 Mpaka Tarehe 06/01/2019.

Akizungumzia Msingi wa ziara hiyo Mhe Mgumba amesema kuwa ni Kukagua Miradi ya Maendeleo inatotekelezwa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Raisi Dkt Jonh Joseph Pombe Magufuli katika jimbo hilo Pamoja na kuhamasiha wananchi Kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya Vyumba vya Madarasa kufuatia ufaulu Mkubwa wa watoto wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwezi huu wa kwanza.

Pia ziara hiyo itakuwa na msingi wa kusikiliza Kero na Changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo anaowawakilisha ili kwa kushirikiana nao Pamoja na  Serikali yao kuzipatia ufumbuzi na kuzitatua.

Alisema kuwa Mafanikio hayo ya ufaulu mzuri wa wanafunzi umeleta changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 17 katika kata Saba kwenye tarafa za Mkuyuni na Ngerengere. shule hizo Mkuyuni Vyumba 7, Kinole 2, Kiroka 2, na Tomondo 3 kwenye tarafa ya Mkuyuni na Ngerengere Vyumba 3, Kidugalo 2 na Tununguo 1.

Pia katika ziara hiyo Mhe Mgumba amepata fursa ya Kutembelea Kituo cha Afya Mkuyuni kujionea hali ya ujenzi unavyoendelea.

Pichani Mhe Mgumba akiwa na Mhr Diwani wa kata hiyo Mhe Mwinyi Buyi na viongozi wengine wakikagua hali ya ujenzi huo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com