Mashine (Mammography) ya uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ya Matiti.
Mtaalam wa Radiolojia Mr Henry Mwansasu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa akimchunguza mgonjwa kwa kutumia mashine (ultrasound).
……………….
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kupitia
kliniki yake ya kinamama wajawazito na uzazi imeanzisha huduma maalumu
ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi (Cervical Cancer) kwa siku
za Jumanne na Alhamisi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na
Uzazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt, Caroline Damian, anasema BMH
imeanzisha huduma hiyo ya bure ya uchunguzi wa saratani kutokana na
kuongezeka kwa tatizo.
“Zaidi ya asilimia 80 ya wanaokuja
hospitalini kwa ajili ya matibabu ya saratani ya mlango wa kizazi,
wanakuja katika hatua za mwisho za ugonjwa. Ndio maana tumeona umuhumu
wa kuanzisha uchunguzi wa bure ili kubaini tatizo katika hatua za
awali,” alisema.
Alisema saratani ya mlango wa kizazi
inasabibishwa na kirusi cha binadamu cha Papilloma (Human Papilloma
Virus), akibainisha kuwa kirusi hicho kinachangia kwa asilimia 99 ya
maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa upande wake, Dkt Caroline Mrema,
ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Hospitali ya
Benjamin Mkapa, ametaja tiba za saratani kuwa ni pamoja na upasuaji
katika hatua za awali za ugonjwa huo, mionzi na dawa kwa kutumia dripu.
“Tiba hizi hazitolewi zote kwa wakati
mmoja kwa mgonjwa. Bali hutolewa kutokana na hatua za saratani, afya ya
mama na umri wake,” alisema.
Akitolea ufafanuzi juu ya tiba ya mionzi,
Dkt Mrema, alisema kumekuwa na fikra potofu juu ya tiba ya mionzi kuwa
ina madhara, akisema tiba hii haina madhara wala haisababishi kifo kama
ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.
0 comments:
Post a Comment