METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 3, 2019

Mhe Juma Ali Khatib aweka jiwe la msingi kituo cha mafunzo ya mbogamboga, matunda na viungo

Waziri asiye  na wizara maalum  Juma  Ali Khatib amewataka  wakulima kujipanga na kuzidi kuwa karibu na wataalamu wa kilimo ili nguvu za wakulima na mahitaji yao  yaweze  kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo ya  nchi .
Akiweka jiwe la msingi kituo cha mafunzo  ya mbogamboga  ,matunda na viungo  (taha)  waziri huyo huko katika uwanja wa kwa binti hamrani mpendae  wilaya  ya mjini unguja  amesema kuwa  endapo kama  wakulima hao  wataweza  kuwa karibu na  wataalamu  basi   wataweza  kuzalisha mazao  yaliyobora na  hata  kupata masoko nje ya nchi ya Zanzibar .
Aidha Ndg  Juma  amesema  kuwa kukamilika kwa kituo hicho  kutaweza    kutimiza mambo ya msingi  ikiwemo  kuweza  kuzalisha zaidi  ya mazao ya mbogamboga, kuzalisha matunda kwa wengi  na hata hivyo  kutoa  fursa za ajira kwa vijana waliowengi  hapa nchini .
Naibu katibu mkuu  wizara  ya kilimo maliasili,mifugo na uvuvi Zanzibar  ahmad kassim   haji  ameeleza  kuwa  wizara  ya kilimo itaendelea na juhudi zake za kuelimisha wakulima katika kutunza uzalishaji  wa  mazao  na  kuhakikisha kuwa  masoko  ya uhakikika yanapatikana  kwa  manufaa  ya wakulima  .
Akisoma risala ya jumuiya  ya Taha  meneja  wa jumuiya hiyo  omari  abuubakar  mohd   amesema kuwa  lengo kuu   la jumuiya  hiyo  ni kuweza kutoa taaluma kwa jamii ili waweze kujikita katika masuala ya kilimo hapa nchini .
Akitoa neno  la shukrani mkuu wa wilaya ya mjini marina joel Thomas  ametoa wito  kwa wananchi  kudumisha amani  na mapinduzi ya nchi  na huku akiwataka wanafunzi wa chuo cha kizimbani kuitumia elimu hiyo ipasavyo ili kuweza kujiajiri wenyewe kwa wenyewe na kutongoja ajira kutoka serikalini .
Na  ishraa  seif  ali 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com