Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi ( wa pili kushoto), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ( wa pili kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa kwanza kulia) wakiwa katika kikao na wataalam wa Tanzania (hawapo pichani) wanaohusika na majadiliano ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Kikao kati ya Mawaziri na Wataalam mbalimbali kutoka Tanzania waliohudhuria Mkutano kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala-Uganda.
Kikao
cha Nne cha Mawaziri mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wanaohusika na
utekelezaji wa mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga
Tanzania kinatarajiwa kufanyika leo jijini Kampala ambapo Mawaziri hao
wanatarajiwa kupata taarifa za majadiliano yaliyokuwa yakifanyika kati ya Timu
ya Kitaifa ya Majadiliano (GNT) ya Tanzania na Uganda ambayo yalianza Januari
21, 2019.
Kutoka
Tanzania Mawaziri watakaohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
Aidha
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia watahudhuria kikao hicho,
hii ni baada ya kufanya kikao jana na Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali
nchini Uganda wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo hivyo Makatibu Wakuu hao
ndio wataokawasilisha taarifa kwa Mawaziri kuhusu majadiliano ya
wataalam wa pande zote.
Kabla
ya kufanya kikao na Mawaziri wa Uganda, Mawaziri hao kutoka Tanzania mapema leo
walifanya kikao na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini
Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi huo ili
kupata taarifa ya awali ya hatua ya majadiliano.
Baada
ya kupata taarifa ya hatua ya majadiliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo
mbili, Mawaziri hao watajadili taarifa hiyo na endapo wataiafiki, hatua
nyingine za majadiliano zitaendelea ambazo sasa
zitahusisha Serikali ya Uganda na Tanzania na wawekezaji wa mradi ambao ni
kampuni ya Total E&P ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, CNOOC
ya China na kampuni za Mafuta za Taifa za Tanzania na Uganda.
Bomba
la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania litakuwa na urefu wa
kilometa 1445.
0 comments:
Post a Comment