Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa, wengine pichani ni Rais Felix Tshisekedi pamoja na Joseph Kabila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa
upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya
maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.
Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za
kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.
“Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa
nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia
na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa
Rais.
Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi
alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa
ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura
milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na
takribani kura milioni 4.4.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza
tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani.
0 comments:
Post a Comment