Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Juma S. Mkomi akipokea Vifaa Tiba vya kujifungulia wakina mama kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki Bi. Aikansia Muro ikiwa sehemu ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais katika kuboresha huduma ya afya ya Mama na Mtoto leo katika hospitali ya rufaa ya Morogoro ambapo Makamu wa Rais alitoa zawadi kwa watoto 36 waliozaliwa tarehe 27, Januari kama kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Lucy Nkya akionyesha juu moja ya mabeseni yenye mahitaji muhimu kwa watoto waliozaliwa leo kama ishara ya kumshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto 36 waliozaliwa leo tarehe 27, Januari ikiwa ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Januari 27 kwa kushirikiana na Benki ya NMB,
wametoa Vifaa Tiba vya kujifungulia katika wodi ya Mama na Mtoto, pamoja na
vifaa tiba hivyo aliwazawadia watoto 36 waliozaliwa siku
ya katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro .
Makamu wa Rais aliwakilishwa na Katibu wake Bw.
Juma S. Mkomi ambaye amesema kuwa Makamu wa Rais amekuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto inaboreshwa.
“Suala la kuboresha huduma ya mama na
mtoto limeelezewa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 lakini
Makamu wa Rais kwa upekee amelipa kipaumbele kwa sabau ni moja kati ya ahadi
zake kuu wakati kampeni” alisema Katibu huyo wa Makamu
wa Rais.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mganga Mfawidhi wa
hospitali hiyo Dkt. Rita Lyamuya amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuwakumbuka
watoto waliozaliwa hospitalini hapo ambapo alisema kuwa watoto 36 wamezaliwa
katika siku ya leo na kwa kipindi cha robo mwaka watoto 1779 walizaliwa kati
ya hao waliozaliwa kwa upasuaji ni 586.
Aidha, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki
Aikansia Muro amesema Benki ya NMB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu
ya tano katika kuboresha huduma zote za kijamii hususani sula zima
la afya na elimu na wataendelea kushirikiana na Serikali katika
kuboresha huduma za kijamii ambapo leo wamemuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais kwa
kutoa Vitanda vinne vya kujifungulia, Vifaa vya kumsaidia mama kujifungulia
(delivery kit) 8, pamoja na vifaa vingine ambavyo kwa ujumla vinagharimu
shilingi milioni 5.
Kwa Upande mwingine Katibu Tawala wa mkoa wa
Morogoro Bw. Clifford Tandari ameishukuru Serikali kwa kutenga
shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 3 na vituo vya afya 11
katika mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment