Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza kikao
alichokiitisha cha Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri
Mkuu, TAMISEMI, Nishati, Maliasili na Utalii, Fedha, Katiba na Sheria na
Viwanda Biashara na Uwekezaji. Wengine walioshiriki katika kikao hicho ni
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, TANESCO, REA na
TFC. Kikao hicho kilifanyika ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Januari
7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amesema kampuni zote zinazosambaza nguzo za
umeme zinatakiwa zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo amboa ni
asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha
za Serikali za Mitaa.
Ametoa agizo hilo leo
(Jumatatu, Januari 7, 2019) baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New
Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu
kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila
nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa
kuzuia nguzo hizo zisitoke.
Wiki iliyopita akiwa katika
ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa
kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa,
Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa
halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.
Viongozi wengine
waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemevu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri Ofisi ya Rais -
TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu
Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya
pamoja na maafisa wengine wa Serikali.
Amesema
lengo la kikao hicho lilikuwa kupata ufafanuzuzi kuhusu malalamiko
yaliyotolewa dhidi ya uongozi wa mkoa wa Iringa kuhusu kuzuia usafirishaji
wa nguzo za umeme zinazotomika kwenye miradi ya Kusambaza Nishati ya
Umeme Vijiji (REA).
Baada
ya kupata maelezo hayo, Waziri Mkuu amemuagiza mkuu wa mkoa wa Iringa
kuiandikia bili kampuni ya New Forest ili ilipe ushuru huo kuanzia Julai 2018
walipoanza kusambaza nguzo. Asilimia 90 ya nguzo za
umeme nchini zinatoka Iringa. Tanzania ina viwanda tisa vya
kutengeneza nguzo na kati ya viwanda hivyo vinane vipo Iringa na kimoja kipo
Tanga.
Kampuni ilizuiwa kutoa
nguzo ndani ya mkoa wa Iringa tangu Novemba 2018 hadi Januari 2019 huku
ikitakiwa kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo ambapo
ilikaa ikitaka iendelee kulipa sh. 5,000 kwa kila nguzo kama walivyokubaliana
na TANESCO jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hata
hivyo, nguzo za umeme ambazo zilikuwa zimezuiwa kwa muda mrefu katika maeneo ya
uzalishaji hususani mkoani Iringa na kusababisha kukwama kwa baadhi ya miradi
ya usambazaji umeme kwenye baadhi ya mikoa nchini juzi zimeanza kusambazwa huku
taratibu nyingine za malipo zikiendelea.
0 comments:
Post a Comment