METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 10, 2019

AKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi kuashiria zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar limekamilika, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud, makazi hayo yanajengwa katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia Vikosi vyake katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais ametoa pongezi zake leo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mkoroshoni Chake Chake Pemba.

Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ni sehemu ya shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ambayo kilele chake itakuwa Jumamosi tarehe 12 Januari, 2019.

“Sote tutakumbuka kuwa wakati wa kupigania uhuru wetu Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kiliwaahidi wananchi wake kuwajengea makaazi bora yenye heshima ya utu. Ahadi za ASP zimerithiwa na Chama cha Mapinduzi na ndio maana leo hii tupo hapa kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la makazi bora ya mwananchi mwenzenu, kiongozi wetu, Makamu wa Pili wa Rais”. Alisema Makamu wa Rais.

Ujenzi huo wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.

Kwa Upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali imeweka umuhimu katika kujenga makazi ya watumishi wake pamoja na Ofisi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com