Na Mwandishi wetu
Katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu kwa ufanisi zaidi
taasisi ya Pamoja Foundation kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA
Foundation imezindua hostel kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule za
serikali.
Uzinduzi wa hostel hiyo uliogharimu jumla ya shilingi
milioni 50 umefanywa leo na Diwani wa Kata ya Tuangoma Mohamed
Suleiman kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbagala Ally Mangungu katika eneo la
Mzinga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hostel hiyo, Diwani wa Kata ya
Tuangoma Selemani amepongeza ubunifu uliofanywa na taasisi ya
Pamoja foundation kwa kuanzisha mradi wa kusaidia wasichana hasa katika masuala
ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine kushirikiana katika kusaidia masuala ya
elimu ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Aidha, aliwaasa wananchi wengine kuiga mfano wa mwananchi wa
eneo la Mzinga kwa kutoa eneo la wakfu kwa ajili ya kujengwa hostel
hiyo ambapo alisema uamuzi huo utawezesha kujenga hostel nyingi na
kubainisha kuwa eneo la Tuangoma ulipo mradi wa viwanja 20000 yeye
kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mbagala ataangalia namna ya kupata
kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hostel kwa kuwa katika mradi huo kuna maeneo
yametengwa kwa ajili ya shule.
Diwani huyo wa kata ya Tuangoma alizishauri taasisi nyingine
kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na
masomo katika fani mbalimbali katika eneo la uchumi ili baadaye nao
waweze kusaidia watu wengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Pamoja Foundation Haji Mrisho
alisema hostel iliyozinduliwa yenye uwezo wa kuwatunza wanafunzi 40
itajulikana pia kama Kituo cha Kuendeleza Wanafunzi ni kwa ajili ya
wanafunzi wa shule za serikali.
Kwa mujibu wa Mrisho, uamuzi wa kuanzisha hostel hiyo unatokana
na utafiti uliofanywa na taasisi yake katika wilaya za Ilala, Temeke na
Kigamboni kuonesha wanafunzi wanaoishi shule za bweni wanafanya vizuri
ukilinganisha na na wale wa shule za kutwa.
Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation alisema, kiwanja
ilipojengwa hostel ni kiwanja kilichotolewa wakfu na kubainisha bila msaada huo
ingekuwa vigumu kuamilisha mradi huo lengo kuunga mkono juhudi za
ardhisetikali elimu bure na kuhamiasisha kuunga mkono Serikali kwa kuwa
wadau wanaweza kusaidia aidha kwa maabara, hostel ama madarasa.
Alisema Taasisi yake imeanzisha hosteli hiyo ikiwa ni jitihada
za kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure na mwakani
taasisi hiyo inatarajia kuanzisha hostel ya wavulana sambamba kuwa na kituo cha
mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha watakaoshindwa kuendelea na masomo
katika viwango tofauti kupata taaluma zitakazowasiadia kimaisha.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation, mbali na
makazi wanafunzi watakaoishi katika hostel hizo watapatiwa elimu,vifaa
mbalimbali vya kujisomea pamoja na mpango wa afya ili wasihangaike katika
masuala ya elimu.
Mrisho alibainisha kuwa, awali taasisi ya Pamoja Foundation
ilikuwa na mpango wa kupanga jengo kwa ajili ya hostel lakini kupatikana
kwa jengo la kudumu kumewapa faraja kubwa kwa kuwa sasa wamepata mradi wa
kudumu.
Mrisho alisema, lengo Ia uanzishwaji hostel ya wasichana kwa
wanafunzi wa shule za Serikali ni kuwawezesha kusoma vizuri hasa ikizingatiwa
watoto wa kike wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo majukumu mengi
wanapokuwa majumbani ukilinganisha wavulana.
Mlezi wa Kituo cha Malezi cha Ibnu Jazar kilichopo Vikundi Picha
ya Ndege Dar es Salaam Mfaki Mohamed alishauri wasichana watakaopata fursa ya
kukaa katika hosteli hiyo kutunzwa vyema ikiwa ni pamoja na wale watakaokuwa na
jukumu la kuwalea kuzungumza nao katika njia iliyo bora na
kuachana na ile dhana ya kuona kuwa viboko kama njia pekee ya
kuwalea wasichana ama wanafunzi na kusisitiza ulelewaji mzuri kwa
wasichana basi kutaepusha mzozo.
Kwa mujibu wa Mfaki kwa sasa kuna adui mazingira kwa
wasichana ambapo kumekuwa na vishawishi vinavyorudisha nyuma wasichana hasa
katika masuala ya maadili na kushauri njia bora ya kukabiliana na hali
hiyo ni kuwandaa wasichana kimaadili ili kuepukana vishawishi
mbalimbali kwa wale watakaopata fursa katika hosteli hiyo.
0 comments:
Post a Comment