Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Katikati) amesimikwa Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa, Tarehe 22 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018.
Baadhi ya Machief Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.
Baadhi ya wananchi Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe.
Na
Mathias Canal, Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani
Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) amesimikwa
kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake
sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa.
Mhe Hasunga amesimikwa kuwa Chief
na Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda wakati akizungumza
na wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika
viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.
Sambamba na kusimikwa kuwa Chief
Nzunda vilevile amekabidhiwa silaha za jadi ikiwemo mkuki wa kujilinda na
maadui kutoka kwa Chifu huyo wa Mbozi.
Akihutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza kwenye mkutano huo, Mhe Hasunga amewashukuru wananchi hao kwa kumchagua
kuwa mbunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi wa Octoba 25, 2015 jambo lililompelekea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kumteua
kuhudumu katika Wizara muhimu nchini ya Kilimo.
Alisema
ushindi wake katika kiti cha ubunge ulisababishwa na imani kubwa ya wananchi kwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani pamoja na
changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi na serikali ya Awamu
ya tano lakini CCM Pekee ndicho kitakachowaletea maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi
na Kisiasa hivyo wananchi wanapaswa kuendelea Kukiunga mkono.
"Huu ni muda wa kuungana na Rais katika kuhakikisha nchi
inasonga Mbele kijamii na kiuchumi, Itikadi za kidini, Kisiasa na kikabila
zinapaswa kuwekwa kando kwa maslahi mapana ya Taifa" Amesema Mhe Hasunga na kuongeza kuwa
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli anatuhimiza
kufanya kazi kwa bidii na hivyo ili kupambana vizuri katika hali zetu kiuchumi
ni wazi kuwa lazima tukubali kuweka siasa kando"
Mhe
Hasunga ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo
silaha pekee ya maendeleo huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea kuimarisha
upatikanaji wa masoko ya mazao hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha kwa bidii
mazao mbalimbali ya kibiashara.
Aidha,
ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko ya wakulima kuhusu bei za pembejeo za
kilimo ili kuwa na unafuu wa gharama zitakazoendana na uwezo wa wananchi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment