Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt
Hamisi Mwinyimvua (katikati) akiongoza kikao kati ya watendaji wa Wizara ya
Nishati na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA).
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua ameongoza kikao kati ya Wizara ya
Nishati na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la
Japan (JICA_) kilicholenga kujadili Mpango wa
uendelezaji wa matumizi ya Gesi Asilia nchini (Domestic Natural Gas Promotion
Plan - DNGPP_).
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi
wa Wizara ya Nishati jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Petroli
na Gesi, Mwanamani Kidaya, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Fortunatus
Mlwanda na maofisa kutoka Idara ya Petroli na Gesi na
Sera na Mipango. Ujumbe wa JICA uliongozwa na Kensuke Kenekiyo.
Ujumbe huo wa JICA uliwasilisha
matokeo ya utafiti wa mahitaji ya gesi asilia uliofanywa katika Miji ya Arusha,
Moshi, Morogoro, Dodoma na Tanga chini ya ufadhili wa Shirika hilo
na kuhusisha wataalam kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC).
JICA wameeleza kuwa zipo njia mbadala
za kufikisha Gesi asilia katika Miji hiyo tofauti na njia iliyozoeleka ya
kujenga bomba ambapo njia zilizoainishwa ni pamoja na kutumia mitungi yenye
gesi iliyokandamizwa (Compressed Natural Gas - CNG_); kujenga mitambo
midogo ya kubadili gesi kuwa kimiminika ( _mini - LNGs_) kisha
kuisafirisha kwenda miji husika au kwa njia ya mitungi ya petroli iliyogeuzwa
kimiminika ( _Liquefied Petroleum Gas - LPG_)
Aidha, JICA imewasilisha uchambuzi wa
kiuchumi unaoonesha gharama za kufikisha gesi asilia katika miji tajwa kwa
kutumia bomba ukilinganisha na njia nyingine kama vile CNG, mini - LNG na LPG.
Kazi hiyo ya utafiti wa mahitaji ya
gesi asilia katika miji tajwa inatarajiwa kukamilika rasmi mwishoni mwa mwezi
Desemba 2018 ambapo taarifa kamili itawasilishwa serikalini.
Katibu Mkuu aliipongeza JICA
kwa utafiti huo na kuwashauri kuhusisha utafiti wao na namna ambavyo ujenzi wa
bomba la gesi asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda utasaidia katika usambazaji
na matumizi ya gesi katika mikoa itakayopitiwa na Bomba hilo.
0 comments:
Post a Comment