Waziri wa Madini Angellah
Kairuki(katikati) Naibu Waziri Stanslaus Nyongo (kulia) na Naibu Waziri wa
Madini Doto Biteko wakifuatilia kikao kati ya wizara na Mkandarasi SUMAJKT anayejega vituo vya
umahiri maeneo mbalimbali nchini na Washauri Elekezi Kampuni za Y&P
Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujenzi wa
vituo hivyo. Kikao hicho kilijadili maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo.
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara
wakifuatilia kikao hicho.
Na Asteria
Muhozya, Dodoma
Waziri wa Madini Angellah Kairuki
tarehe Novemba 8, aliongoza kikao cha kujadili Maendeleo ya Ujenzi wa Vituo vya
Umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali nchini.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na
Naibu Mawaziri Stanslaus Nyongo na Doto Biteko pamoja na Menejimenti ya Wizara
ambapo Mkandarasi SUMAJKT na Washauri Elekezi kampuni za Y&P Architects,
InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujezi wa vituo hivyo walieleza
kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa za ujenzi wa vituo hivyo.
Vituo vya umahiri vinajengwa maeneo
ya mbalimbali nchini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
(SMMRP) ulio chini ya wizara.
Vituo hivyo vinalenga katika kutoa
mafunzo ya jiolojia katika utafiti wa madini, mafunzo ya uchenjuaji wa madini
kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia
zebaki.
Vilevile, vinalenga katika kutoa
mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo wa madini, mafunzo ya usalama na afya
sehemu za kazi na mafunzo ya namna bora za utunzaji wa mazingira kwenye migodi
ya wachimbaji.
Akizungumza katika kikao hicho,
Waziri Kairuki alisisitiza kuhusu kuzingatiwa kwa ubora wakati wa ujenzi wa vituo husika na kusisitiza
Mkandarasi SUMAJKT kukamilisha ujenzi huo katika muda uliopangwa.
Vituo vya umahiri viko katika hatua
mbalimbali za ujenzi na vinajengwa Bariadi, Bukoba, Handeni, Musoma, Songea, Chunya,
Mpanda na Chuo Cha Madini Dodoma.
Ujenzi wa vituo hivyo utagharimu
kiasi cha shilingi Bilioni 11.9
zinazotokana na mkopo wa Benki ya Dunia.
0 comments:
Post a Comment