Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka
Jiwe la Msingi la Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe,
Novemba 29, 2018. Kulia ni Mbunge wa Bukombe na Naibu waziri wa Madini, Doto
Biteko na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert
Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanakwaya wa Ushirombo wakiimba wakati Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia Mkutano wa hadhara kwenye Stendi ya
Ushirombo, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi
wote wa umma wakiwemo wa kada ya afya kupitia Bodi ya Mishahara na Motisha baada
ya kukamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi.
Amesema
kukamilika kwa uhakiki huo wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma
kutaiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
kupanga upya mishahara na motisha kwa watumishi.
Waziri Mkuu
alitoa taarifa hiyo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na
watumishi wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe baada ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji miundombinu wa kituo hicho uliogharimu
sh. milioni 500.
Alisema
Serikali inaendelea kushughulikia maslahi ya watumishi, hivyo aliwataka
waendelee kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
“Tunataka mwananchi akifika kwenye maeneo ya kutolea huduma apokelewe, asikilizwe
na ahudumiwe.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya
Bukombe kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika
kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo imebakisha vijiji 2 kati ya 52 kumalizia
ujenzi huo.
Waziri Mkuu
alisema kwa sasa wananchi wa Ushirombo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu
hadi Geita mjini au wilayani Kahama kwa ajili ya kufuata huduma za afya kwa
kuwa huduma zote zitakuwa zikipatikana kituoni hapo.
Alizitaja
huduma ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye Kituo cha Afya cha Ushirombo kuwa ni
pamoja na za mama na mtoto, huduma za upasuaji wa aina zote mdogo na mkubwa,
maabara, chumba cha kuhifadhia maiti.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Dionis Myinga
alisema ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo ulianza Juni 22, mwaka huu na
unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Alisema lengo
la mradi huo ni kukiwezesha Kituo cha Afya cha Ushirombo kutoa huduma bora za
upasuaji wa dharura kwa akinamama wajawazito pindi wapatapo matatizo yatokanayo
na uzazi. Majengo yote ya kipaumbele yamekamilika kwa asilimia 99.
“Mradi huu
ambao tunaujenga kwa kutumia force account, pamoja na lengo la kutatua matatizo
yatokanayo na uzazi kwa akinamama mradi huu utakapokamilika, Kituo cha Afya cha
Ushirombo kitaweza kuhudumia watu wapatao 54,271.”
Mkurugenzi huyo
alisema mradi wa ukarabati wa kituo hicho cha afya unakadiriwa kutumia sh.
milioni 436.933 hadi utakapokamilika na sh. milioni 63.066 zilizosalia kwenye
ukarabati huo zitatumika kujenga njia za kuunganisha wodi na kukarabati majengo
ya zamani.
0 comments:
Post a Comment