Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapoNovemba 28, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Mwl.Anselm Mnibhi wa Shule ya Sekondari Mwembeni ambaye pia alimfundisha yeye akiwa mwanafunzi wa shule hiyo mwaka 1997-2000, wakati wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo, iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wakurya, katika mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alikuwa mgeni rasmi.
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa
walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na
heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa
maadili kwao na wanafunzi wanaowafundisha.
Mtaka
ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule
ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne
mwaka 1997-mwaka 2000), iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Amesema
katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo
yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi
kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.
"
Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha
walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini
shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa
watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii
kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.
Katika
hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa
elimu wakiwemo wanafunzi waliosoma katika shule ya Mwembeni miaka ya nyuma
kuchangia katika ujenzi wa shule(vyumba vya madarasa) ili kupanua wigo kwa
wanafunzi kuanza kusoma masomo ya sayansi, ikizingatiwa kuwa katika dunia ya
sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia.
"Dunia
tunayoiendea sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia na kama shule
imejielekeza kwenye masomo ya sayansi ni jambo la kuungwa mkono; niwaalike
wenzangu wote tuliosoma katika shule ya sekondari Mwembeni kuona haja ya
kurejesha kwenye shule katika kile tulichopata katika shughuli zetu za
kimaisha, tukirejeshe tujenge shule yetu ili iendelee kuwa kwenye ushindani
mkubwa na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Mara" alisisitiza Mtaka.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari
Mwembeni, Bro.Erasmus Marando amewaomba wadau wasaidie kujenga vyumba
zaidi vya madarasa, shule hiyo ianze kutoa masomo ya mchepuo wa sayansi, ili
kuwaanda wataalam watakaoenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano ya
Tanzania ya Viwanda.
Naye
Mwalimu Anselm Mnibhi ambaye amemfundisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni mwaka 1997 hadi mwaka 2000,
amemshukuru kwa kukumbuka shule aliyosoma na kuonesha nia ya kusaidia katika
ujenzi wa vyumba vya madarasa na kubainisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote
aliyesoma hapo zamani aliyeonesha nia na dhamira hiyo na akawaomba wote
waliosoma shuleni hapo kujitoa kujenga shule yao.
Kwa
upande wake mhitimu wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni,
Sharon Buganda ametoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuondokana na dhana ya
kuogopa kusoma masomo ya sayansi wakiamini kuwa ni magumu, badala yake wasome
masomo hayo ili waweze kuwa wataalam wajao katika maeneo mbalimbali
ikiwemo viwanda ambavyo ni sera ya Serikali ya Awamu ya tano.
Katika
mahafali hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aliahidi kuchangia
shilingi milioni tano na kuhamasisha wenzake aliosoma nao shuleni hapo Mwembeni
kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vitakavyotumika na wanafunzi wa
mchepuo wa sayansi, kutoa zawadi ya shilingi milioni moja (kwa mwanafunzi wa
kiume) na shilingi milioni moja na laki tano(kwa mwanafunzi wa kike)
atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa katika mtihani wa
Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment