Moja ya eneo lililonufaika na mfumo wa majitaka ujulikanao kama ‘Simplified Sewerage’. Pichani ni Mtaa wa Unguja, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza ambao ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na mradi wa majitaka wa simplified sewerage kupitia ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akikagua ubunifu uliotumika katika ujenzi wa mradi wa majitaka, Mabatini mtaa wa Unguja wilaya ya Nyamagana. Mradi huo umejengwa kwenye maeneo ya miinuko na umesaidia kuondosha uchavuzi wa mazingira na magonjwa ikiwamo Kipindupindu.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (mbele) akiwaongoza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Mjini Moshi (MUWSA) eneo la Mabatini Jijini Mwanza walipotembelea kujifunza mfumo wa majitaka Oktoba, 2018. Ni mradi wa kipekee kuwahi kutekelezwa nchini.
Moja ya eneo lililonufaika na mfumo wa majitaka ujulikanao kama ‘Simplified Sewerage’. Pichani ni Mtaa wa Unguja, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza ambao ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na mradi wa majitaka wa simplified sewerage kupitia ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).
Mradi wa Majitaka unaotekelezwa kwenye maeneo ya
miinuko Jijini Mwanza unaofahamika kama "Simplified Sewerage" umekuwa
miongoni mwa miradi miwili bora zaidi kuwahi kutekelezwa Barani Afrika
chini ya ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).
Hayo yameelezwa mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2018
wakati wa Mkutano wa kujadili miradi inayofadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kupitia mfuko huo wa EU-AITF.
Katika mkutano huo ilielezwa kwamba tangu mfuko huo
uanzishwe mnamo mwaka 2007 ni miradi miwili pekee ambayo imefuzu na kuwa miradi
bora zaidi kuwahi kutekelezwa ambayo ni Mradi wa Majitaka wa Simplified
Sewerage wa Jijini Mwanza, nchini Tanzania na mwingine ni mradi wa Nishati ya
Umeme wa Benin & Togo.
Akizungumzia mradi wa Majitaka wa Jijini
Mwanza, Mshauri wa masuala ya Kiufundi wa Benki ya
Uwekezaji ya Ulaya, Raoul Pedrazzani alielezea hali ilivyokuwa hapo awali kabla
ya kujengwa kwa mradi mpya wa majitaka kwenye maeneo ya milimani jijini humo.
Pedrazzani alisema kuwa kijiografia maeneo mengi ya
Jiji la Mwanza ni milima/miinuko na kabla ya mradi huo wa majitaka wakaazi wa
maeneo ya milimani hawakuwa na mfumo mzuri wa uondoaji wa majitaka hali ambayo
iliwasababishia adha mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa mazingira na maradhi.
Alisema suluhisho ilikuwa ni kubuni mradi ambao
utarahisisha utoaji wa majitaka kutoka kwenye makazi hayo kwenda yanakostahili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga
alithibitisha kupokea ujumbe wa pongezi juu ya ushindi huo.
Mhandisi Sanga aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya
MWAUWASA kwa usimamizi mahiri wa shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka na pia
aliwapongeza watumishi wote wa MWAUWASA kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa
miradi husika. “Mungu ni Mwema, tunamuomba Aendelee kutusaidia. Hakika kwa
pamoja tunaweza,” alisema Mhandisi Sanga.
Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha
huduma ya majitaka inapanuka zaidi ili wananchi walio wengi waweze kufikiwa.
Maeneo ya miinuko ambayo tayari yamefikiwa na mfumo
huo wa Simplified Sewerage ni Kilimahewa, Mabatini na Igogo na huku lengo
likiwa ni kupanua wigo na kufikia maeneo mengi zaidi.
0 comments:
Post a Comment