Inaeleweka kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, Lakini pia madhara mengine yatokanayo na unywaji wa pombe uliokithiri ni kusababisha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Muwezeshaji wa semina Mwalimu Kandi Mbwambo akitoa ufafanuzi wa jambo kwa washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS).
Hayo yameelezwa
mapema wiki hii na Mwalimu Kandi S. Mbwambo ambaye ni muwezeshaji kutoka Kituo
cha Walimu Sinza (TRC) alipokuwa akiwasilisha mada inayosema ukatili wa
kijinsia kwa wanawake na watoto kama matokeo ya unywaji pombe (ulevi).
Mwalimu
Mbwambo alisema kuwa imezoeleka kuonekana kwa mzazi wa kiume akilewa pombe anakuja
kuanzisha vurugu nyumbani kwa kupiga mke na watoto na jamii kumchukulia kama
mlevi na kusahau kuwa kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.
Aidha
aliendelea kusema kuwa ukiachia mbali vurugu lakini pia mlevi anaweza
kutekeleza vitendo vingine visivyotarajiwa katika jamii kama kubaka na
kulawiti watoto, kujikojolea na hata kutokwa na haja kubwa kwa wakati mwingine hali
inayofanya heshima yake kushuka ndani ya jamii.
“Lakini pia
kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yake kwani anaweza kupata madhara
ya kiafya ikiwemo kupata magonjwa kama TB, Mapafu kushindwa kufanya kazi kutokana
na kunywa pombe kali, Na kwa muda mwingine hata kufanya ngono zembe hali inayoweza
kusababisha kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo Virusi Vya Ukimwi” alisema Mwalimu
Mbwambo
Alisisitiza
kuwa Mababa wengi wakishaanza unywaji wa pombe wanakuwa na matumizi makubwa ya
pesa katika pombe na kusahau familia zao na wengine ufikia hata kutelekeza
familia zao ama kukimbiwa na wenzi wao kutokana na kushindwa kutimiza majukumu
yao ipasavyo.
Na baadhi ya
wananchi walitoa maoni yao kuhusiana na nini kifanyike ili kupunguza
madhara haya yatokanayo na pombe, Na wengi wao walisisitiza kuwa kupunguzwa kwa muda wa
unywaji pombe ikiwezekana iwe ni kuanzia saa 12jioni mpka saa 2 usiku labda
inaweza kusaidia.
“Lakini pia
serikali kutekeleza sharia walizoziweka juu ya udhibiti wa Bar na pombe ili
kuweza kuwepo na utulivu katika hili, kwa mfano kuviondoa vilabu holela vyote
vinavouza pombe kinyume na sharia pamoja na kudhibiti uuzaji wa pombe kwenye
maduka ya vyakula”. Walisema washiriki
Na mwisho walipendekeza elimu iendelee kutolewa kwa wananchi juu ya madhara ya pombe, pamoja na kutengeneza
matangazo na kuyasambaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu madhara ya unywaji wa pombe uliokithiri.
Mwalimu Kandi S. Mbwambo akielezea kwa undani jambo fulani mbele ya washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Mapema wiki hii, zinazofanyika kila jumatano katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam .
Semina ikiendelea
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Semina ikiendelea mapema wiki hii Makao Makuu ya TGNP Mtandao.
0 comments:
Post a Comment