Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia kutumia kifaa maalum ili kujua kiwango cha madini ya Bati bati katika kiwanda cha TanzaPlus Minerals alipotembelea kiwandani hapo. Kiwanda hicho maalum kwa ajili ya shughuli za uchenjuaji madini ya bati kinamilikiwa na Mtanzania Salim Mhando (Diaspora)
Jengo la Kituo cha Umahiri cha Bukoba katika hatua za ujenzi
Mmiliki wa kiwanda cha kuchenjua madini ya bati cha TanzaPus Minerals, Salim Mhando akimwnesha waziri wa Madini Angellah Kairuki na ujumbe uliotembelea kituo hicho madini ya Bati
Ø Awatoa wasiwasi
wachimbaji wa Bati Kyerwa
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki amemtaka Mkandarasi Kampuni ya SUMAJKT kuzingatia
muda uliopangwa wa kukamilisha ujenzi wa
vituo vya Umahiri vinavyojengwa na
kampuni hiyo maeneo mbalimbali nchini na endapo itashindwa kukamilisha kwa wakati
asahau habari ya kusheherekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo Novemba 19,
wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umahiri cha Bukoba
ambacho ni miongoni mwa vituo vinavyojengwa na serikali ambapo pamoja na mambo
mengine, vinalenga kutoa mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia
rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.
Pamoja
na kupogeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha Bukoba, Waziri Kairuki
ameitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuwezesha majengo hayo kutumiwa na
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo ili kuendelezaji sekta ya madini nchini.
Waziri
Kairuki alisema kuwa, ujenzi wa vituo hiyo umepangwa kukamilika ifikapo disemba
22 mwaka huu na shughuli zote za ujenzi zinatakiwa kukamilika
ifikapo Januari 15, 2019.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Meneja wa Opereshi ya SUMAJKT Kapteni Fabian Bubelwa alisema
kuwa, ujenzi wa kituo cha Bukoba utagharimu shilingi bilioni 1.8 na kilipangwa
kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 6
kama ilivyokubalika katika Mkataba na
kuongeza kuwa, hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 35.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, alimwahidi Waziri
Kairuki kufuatilia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo kutokana na thamani yake
na manufaa yake kwa mkoa huo na kuongeza kuwa, mkoa huo unakionea fahari kituo
hicho.
Katika
hatua nyingine, Waziri Kairuki akizungumza
kwa nyakati tofauti ikiwemo na Wamiliki
wa Kampuni TanzaPlus inayolenga kufanya
shughuli za uchenjuaji wa madini ya bati wilayani Kyerwa , na wachimbaji wa
madini ya bati katika kijiji cha Nyaruzumbura, amewataka wadau hao kuwa
wavumilivu wakati serikali ikikamilisha taratibu za kupata Mkataba wa Hatimiliki ya madini hayo ili yaweze kutambulika katika eneo na nchi
yanayotoka kutokana na upekee wa madini hayo ikiwemo mahitaji yake katika soko
la dunia.
Waziri
Kairuki alisema zipo fursa nyingi zinakuja kutokana na uwekezaji wa madini hayo
na kueleza kwamba, wapo wawekezaji wa kampuni za TanzaPlus ambao walikuwa na
changamoto ya leseni lakini sasa tatizo hilo halipo tena.
“ TanzaPlus na ATM wanatarajia kununua kiasi
kikubwa cha madini ya bati kutoka kwenu kwa hivyo muwe wavumilivu fursa zipo.
Na wanasema wanahitaji kiasi kikubwa sana huenda hata kiasi mnachochimba
kisiwatosheleze, alisema Kairuki.
Aidha,
alitumia fursa hiyo kumpongeza Meneja na mmiliki wa kiwanda cha TanzaPlus
Minerals Salim Mhando ambaye pia ni Diaspora kwa jitihada zake za kuanzisha
kiwanda cha uchenjuaji wa madini ya bati nchini na kueleza kuwa, kitakuwa
kiwanda cha kwanza cha uchenjuaji wa madini ya bati nchini.
Mbali
na kiwanda hicho, Wilaya ya Kyerwa pia inatarajiwa kuwa na kiwanda kingine cha uchenjuaji wa
madini ya bati cha ATM ambacho kinatarajiwa kuanza shughuli zake ifikapo mwezi
Machi mwaka 2019 ilihali kiwanda cha TanzaPlus Minerals kinatarajiwa kuanza
shughuli za uchenjuaji mwezi Januari mwaka ujao.
Akizungumzia
kuhusu manufaa ya madini hayo, amewataka wamiliki hao kuzingatia na kufuata bei
elekezi zinazotolewa na Serikali na kueleza kuwa tayari wizara kupitia Tume ya
Madini imeanza kutoa bei elekezi za madini suala ambalo wadau wa madini wanatakiwa kulizingatia.
Vilevile,
Waziri Kairuki aliendelea kusisitiza kuhusu
zuio la kusafirisha madini ghafi nje ya nchi kabla ya kuongezwa thamani na kueleza kwamba, uongezaji thamani madini
nchini unalenga katika kuwanufaisha wachimbaji na taifa ikiwemo kuhamasisha
viwanda vya ndani.
Pia,
aliwaeleza wachimbaji hao kuwa, pale
ambapo shughuli za uzalishaji wa madini hayo zitakapokaa vizuri wanapaswa
kuzingatia ulipaji wa tozo mbalimbali za serikali ikiwemo kuzingatia sheria na
taratibu zote zinazotakiwa katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.
Aliongeza
kuwa, bado wachimbaji wadogo wanachangia asilimia ndogo katika ulipaji kodi
ikilinganishwa na uwekezaji wao pamoja na shughuli za uchimbaji wanazofanya.
Kwa
upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Kagera, Lucas Mlekwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Nyaruzumbura uzalishaji wa madini ya bati, alisema kuwa kuna jumla
ya leseni za uchimbaji mdogo madini hayo 250 zilizopo Wilayani Kyerwa ambapo
leseni 120 ndiyo zina uzalishaji kwa sasa na wa kusuasua.
Baada
ya kukagua maendeleo ya kituo cha Bukoba, katika ziara yake, waziri Kairuki anaendelea
na ukaguzi wa vituo vingine kikiwemo cha Musoma, Bariadi, Handeni, Songea,
Chunya, Mpanda na Songea
Vituo
vya Umahiri vinajengwa na mkandarasi kampuni ya SUMAJKT maeneo mbalimbali
nchini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) na
vinalenga kutoa mafunzo ya jiolojia katika utafiti, mafunzo ya uchenjuaji wa
madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia
zebaki.
Halikadhlika
vinalenga katka kutoa mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo, mafunzi ya
usalama na afya sehemu za kazi na mafunzo bora za utunzaji wa mazingira kwenye
migodi ya wachimbaji.
0 comments:
Post a Comment