Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha
Bupandwampuli wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha
Butarama wilayani Chato mkoani Geita.
Moja
ya nyumba iliyounganishwa na huduma ya umeme katika Kijiji cha Butarama
wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wakazi wa Kijiji cha
Kikumbaitale wilayani Chato kabla ya kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji
hicho.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara wilayani Chato mkoani Geita ya
kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu ( REA III).
Akiwa
wilayani humo amezindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bupandwampuli,
Kikumbaitale na Butarama.
Vijiji
74 wilayani Chato vipo katika mpango wa kupelekewa umeme kupitia REA III ambapo
mpaka kufikia tarehe 27 Oktoba, 2018, Vijiji 20 vimeunganishwa na huduma
hiyo.
0 comments:
Post a Comment