Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dsr es salaam
Oktoba 27, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum
Shamte. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte baada ya kukutana na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali inathamini uwepo wa sekta binafsi nchini na kwamba inaendelea
kushirikiana nayo katika kuboresha maendeleo ya Taifa.
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba
27, 2018) wakati alipokutana na bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
kwenye makazi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ampongeza Mwenyekiti wa
taasisi hiyo Bw. Salum Shamte na wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuingoza
taasisi hiyo. Bodi hiyo mpya ilikwenda kujitambulisha.
“Serikali inadhamira ya dhati ya
kushirikiana na taasisi hii kwa sababu ndio muwezeshaji wa kuifanya Tanzania
kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
taasisi hiyo Bw. Shamte amesema sekta binafsi inatambua juhudi za Serikali
katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania.
“Sisi tupo tayari kushirikiana na
Serikali kwa kuwabana wafanyabiashara ambao wanaenda kinyume na maadili na
sheria, ila tunaomba Serikali ishirikiane nasi katika utekelezaji wake.”
Pia, Bw. Shamte ameiomba Serikali
iendelee kutoa vivutio kwa biashara zinazoanza ili kuhamasisha uwekezaji kwa
kuwa baadhi yake zimeonesha gharama kubwa za uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment