Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza umuhimu wa SACCOS nchini wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya wanachama wa vikundi vya akiba na mikopo wakifatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi (Mb) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Na Mathias
Canal, WK-Iringa
Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Tanzania imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto zinazovikabili
vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vinaleta
tija kwa jamii.
Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na
kuchukua hatua za kiutawala na kidola kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa
vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo waliojihusisha na wizi na ubadhirifu wa
fedha katika vyama hivi, mfano; Alayabe SACCOS cha Karatu Mkoani Arusha, Mbinga Teachers SACCOS
Mkoani Ruvuma na Ulanga Teachers SACCOS Mkoani Morogoro ambako baadhi ya
viongozi na watendaji wamefikishwa mahakamani kwa vitendo vya ubadhirifu.
Vilevile, Kutengeneza mikakati ya kuhakikisha
kwamba vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo haviendelei kutengeneza madeni
yasiyokuwa na tija kwa jamii na kusaidia kuweka mikakati ya kupunguza madeni
ambayo tayari yapo katika vyama vyetu vya ushirika wa Akiba na Mikopo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo
Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya
Saccos Duniani iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe
18 Septemba 2018.
Waziri Tizeba alisema kuwa serikali imeanza
kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na waajiri kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali
kwa ajili ya kuwahimiza waone umuhimu wa kuwasilisha kwa wakati makato
wanayokata kutoka katika mishahara ya watumishi waliokopa katika SACCOS ili
fedha hizo ziweze kutumika kwa shughuli za maendeleo zilizokusudiwa.
Alisema pia, serikali itaendelea kuendesha
mafunzo mbalimbali kwa viongozi, watendaji na wanachama wa vyama vya ushirika
vya Akiba na Mikopo ili waweze kufahamu miongozo na taratibu mbalimbali za
utendaji wa vyama hivi ili hatimaye viweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii
inayozunguka.
Katika utafiti uliofanyika katika siku za hivi
karibuni umebaini kwamba Tanzania ina jumla ya vyama vya ushirika vya Akiba na
Mikopo 5640 kati ya vyama 55000 sawa na asilimia 10.3 ya vyama vya ushirika wa Akiba na
Mikopo Duniani.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania ina jumla
ya wanachama wapatao milioni moja na laki nane kwa SACCOS zote nchini kati ya
wanachama milioni miambili (200) ya
wanachama wote wa SACCOS sawa na asilimia 0.9
ya wanachama wa SACCOS zote Duniani.
Dkt Tizeba alisisitiza kuwa Licha ya uchache
wa wanachama wake ukilinganisha na idadi ya wanachama Duniani, SACCOS hapa
nchini Tanzania zimeendelea kuwa msaada na mkombozi mkubwa katika kuondoa
umasikini wa wanachama wa vyama hivi na jamii kwa ujumla wake.
Aidha, alisema Sekta ya ushirika wa Akiba na
Mikopo (SACCOS) imeendelea kupanuka katika nchini kufuatia kuanzishwa kwa
SACCOS nyingi katika maeneo ya mijini na vijijini hali ambayo imechangia
kuongeza huduma ya kifedha kwa wananchi wa kawaida na hivyo kuleta tija kwa
jamii.
Sambamba na hayo, alieleza kuwa uwepo wa
maendeleo ya ushirika wa Akiba na Mikopo nchini umesaidia wanachama wengi
kujijengea utamaduni wa kuweka akiba ya fedha mara kwa mara na kuwa na matumizi
bora ya fedha wanazoweka akiba. Vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS)
vimechangia kujenga tabia ya kujiamini na kuaminiana kifedha miongoni mwa
wananchi wa kawaida na kujenga.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment