METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 20, 2018

HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUBORESHA MAJENGO CHUO CHA ST. MARK'S KUFANYIKA KESHO JIJINI DAR


Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangisha fedha za maboresho ya majengo ya Chuo cha ST. Mark's Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Agustino Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Harambee itakayofanyika kesho tarehe 20.10.2018 chuoni hapo ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndungai. Kiasi cha Tsh Milioni 800 zinahitajika katika ukarabati wa kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha St. Mark's Dkt. Peter Kopweh akifafanua jambo kuhusiana na harambee hiyo.

Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo ya Chuo cha St. Mark’s kilichopo Buguruni Marapa amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia harambee kwa ajili ya kuboresha majengo ya chuo hicho kiasi cha fedha tsh Milioni 800.

Hayo yalisemwa wakati alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari chuoni hapo ambapo alisema  uamuzi wa kuboresha majengo hayo umetokana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Kuagiza wafanye hivyo.

“Nimewaiteni waandishi wa Habari kwa lengo la kuwataka kutusaidia kuutangazia umma kuwa siku ya jumamosi Octoba 20, 2018 tutakuwa na harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo yetu kama tulivyo agizwa na TCU” alisema Jaji Ramadhani.

Zaidi ya Tsh Milioni 800 zinatarajiwa kuchangishwa katika harambee hiyo itakayofanyika chuoni hapo kuanzia saa nane mchana na mgeni rasmi anatarajia kuwa Spika wa Bunge Job Ndungai. 

Kwa ambao hawatoweza kufika katika harambee hiyo wanaweza pia kuchangia katika njia zifuatazo

TIGO PESA : 0677058716

CRDB BANK: 0150237155300 (HOLLAND BRANCH)

TIB : 004600000860601 (SAMORA DAR ES SALAAM)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com