METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 20, 2018

Hali ya Soko la Mahindi ndani ya EAC ni Gumu kwa Mwaka Huu

Anaandika; Mhe Omary Mgumba, Naibu Waziri wa kilimo

Hii ni  baada ya Nchi nyingi kuzalisha kwa wingi kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri kwa uzalishaji Wa Mahindi katika maeneo mengi.

Pili ni kutokana na  stock za Mwaka  Jana na Pia stock za Importation za Mwaka Jana toka Nchi ya Mexico kwa Baadhi ya Nchi Jirani kutoka na upungufu Mkubwa Wa Mahindi Mwaka uliopita katika ukanda wetu.

Picha ya chini ni hali ya Soko la Mahindi Nchini Kenya kutoka na na Malalamiko ya wakulima na Kamati ya Bunge za hesabu za serikali kuu,  kwa nini CPB ya kwao wanaingiza Mahindi Kenya wakati Mahindi ya Wakenya hayana Mnunuzi na waliouza kwa mkopo wana zaidi ya miezi miwili hawajalipwa.

Bei pia Zinaendelea Kushuka .Nikiwa Huko Tarehe 26/09/2018 siku hiyo ndiyo ya mjadala huu na bei kushua toka 82 KSH kwa Kilo mpaka 75 KSH kwa Kilo .Kwa Bei hizi ni kubwa kuliko za kwetu na ndiyo maana wasagishaji wao wanapendelea kununua Mahindi toka Kwetu na Uganda kutoka na Bei nafuu kiliko ya kwao.

Mwisho Tunaendelea kutafuta Masoko zaidi kwenye Nchi zile zenye upungufu kidogo kama Sudani ya Kusini, Kongo Nk. Ingawa ushindani ni Mkubwa.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com