Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto) akiwasikiliza wachimbaji wa mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani alipofanya ziara katika machimbo hayo kujionea uendeshaji wa shughuli na ulipaji kodi stahiki za serikali.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wamiliki wa leseni ya uchimbaji mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilayani Mkuranga na kukagua vitabu vya ripoti za uendeshaji wa shughuli zake.
Na George Binagi-GB Pazzo
Wachimbaji
wa mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, wamelalamikia
ujio wa mashine za “skaveta” (Excavator) katika machimbo hayo kwa hofu ya
kupoteza nafasi zao za kazi.
Katibu wa
wachimbaji hao, Seleman Zombe anasema hatua hiyo itaathiri wachimbaji wengi
wakiwemo vijana wanaokadiriwa kufikia 1,000 na hivyo kuomba serikali kuzuia
mashine hizo kufanya kazi katika machimbo hayo.
Hayo
yamejiri Oktoba 23, 2018 baada ya Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kufanya
ziara katika machimbo hayo kukagua uendeshaji wa shughuli za uchimbaji mchanga
na ulipaji wa kodi stahiki za serikali.
Hata hivyo
Biteko alishtushwa na madai ya wachimbaji hao na kuwahimiza kuendana na kasi ya
mabadiliko ya teknolojia ambayo inarahisisha utendaji kazi ambapo alishauri
wawekezaji wenye leseni katika machimbo hayo kuweka mikakati bora ya vijana hao
kuendelea kufanya shughuli zao licha ya uwepo ya mashine za “skaveta”.
SOMA>>>Biteko aonya ukwepaji kodi katika machimbo ya Kaolin wilayani Kisarawe
0 comments:
Post a Comment