Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Buddha Mining and Explorers wakati wa kusikiliza na kutatua mgogoro baina ya kampuni hiyo na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd baada ya kufanya ziara katika mgodi wa uchimbaji madini/ mawe ya marumaru Mabo (Mable) mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko akitoa maamuzi baada ya kikao kifupi cha utatuzi wa mgogoro baina ya kampuni ya Buddha Mining and Explorers na kampuni ya anzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ambaye pia ni
mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini akizungumza baada ya Naibu Waziri wa Madini
Mwl. Doto Biteko kutembelea machimbo ya mabo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko (kushoto)
akisalimiana na Mkurugenzi wa mampuni ya Zhong Fa Construction Material Group
Co. Ltd, Alston Zhiling Yi (kulia). Kampuni hiyo inajishughulisha na uchimbaji
wa mawe/ madini ya ujenzi aina ya mable katika Kijiji cha Maseyu Kata ya Gwata
mkoani Morogoro.
Sehemu ya mitambo ya kuchakata madini ya mabo katika eneo la
mgodi wa madini hayo unaomilikiwa na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction
Material Group Co. Ltd iliyopo katika Kijiji cha Maseyu mkoani Morogoro.
Baadhi ya malighafi zitokanazo na madini ya mabo (Mable) zinazotengenezwa
na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd mkoani
Morogoro. Madini haya hutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo "Tiles".
Naibu Waziri
wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko ametatua mgogoro baina ya kampuni ya Buddha
Mining and Explorers na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material
Group Co. Ltd zilizokuwa ziking’ang’ania eneo moja kwa ajili ya shughuli za
uchimbaji madini katika Kijiji cha Maseyu Kata ya Gwata mkoani Morogoro.
Awali
kampuni ya Buddha Mining and Explorers iliomba leseni kwa ajili ya kufanya
utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo na baadae kampuni ya Tanzania
Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd ikabaini uwepo wa madini ya mabo
katika eneo hilo na kuanza shughuli zake bila kuwa na leseni hatua ambayo
iliibua mvutano baina ya kampuni zote mbili.
Alhamisi
Oktoba 11, 2018 Naibu Waziri Biteko alikutana na pande zote mbili, kampuni ya Buddha
Mining and Explorers ilikubali kuachia eneo hilo na hivyo kampuni ya Tanzania
Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd kutakiwa kuomba rasmi leseni ya
uchimbaji madini ya mabo ili ifanye shughuli zake kihalali na kulipa kodi zote
stahiki.
SOMA>>>Serikali yasisitiza msimamo wa kuufunga mgodi wa kokoto wilayani Bagamoyo
0 comments:
Post a Comment