METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 12, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AFUNGUA WARSHA YA MRADI WA KUSAIDIA MAENDELEO YA ZAO LA MPUNGA-TANRICE 2

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akifungua semina ya mradi wa kusaidia maendeleo ya zao la mpunga TANRICE awamu ya pili katika ukumbi wa Umoja Lutheran Hostel Moshi, Leo tarehe 12 Septba 2018.
Washirika wa semina ya mradi wa kusaidia maendeleo ya zao la mpunga TANRICE awamu ya pili wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati akifungua warsha hiyo inayofanyika katika ukumbi wa Umoja Lutheran Hostel Moshi, Leo tarehe 12 Septba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe leo 12 Septemba 2018 amefungua semina ya mradi wa kusaidia maendeleo ya zao la mpunga TANRICE awamu ya pili.

Katibu Mkuu huyo amefungua mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Umoja Lutheran Hostel Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu huyo alisema kwamba kwa miaka mingi Tanzania ilikuwa ikiingiza mchele kutoka nje, lakini hivi karibuni kupitia jitihada mbalimbali wizara ya Kilimo imeweza kujitosheleza kwa mchele na kupelekea kuwa na ziada ya kutosha.

Aliongeza, kuwa kwa mwaka 2017/2018 uzalishaji wa mchele umefikia Tani 2,219,628 na mahitaji ni tani 990,044 hii ina maana kwamba nchi ina ziada ya mchele ya tani 1,229,583. 

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa hali hiyo imefanya kuwa na kiwango cha utoshelevu wa mchele (SSR) kwa asilimia 224%. 

Alisisitiza kuwa ziada hiyo ni sehemu ya matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Wizara ya kilimo ukiwemo mradi huo wa TANRICE awamu ya pili.

Katibu Mkuu Mhandisi Mathew J. Mtigumwe alisisitiza kwamba, Serikali ipo tayari na itaendelea kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia shirika la JICA katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo nchini.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com