Elizabeth Mlanda (kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda akimkabidhi Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka bahasha yenye fedha kama shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu
Elizabeth Mlanda (kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda wa Mjini Bariadi akimkabidhi Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka zawadi ya unga wa ngano, mafuta ya kula na sukari , Agosti 04, 2018,' Mjini Bariadi ikiwa ni shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Bibi.
Elizabeth Mlanda Mke wa Mfanyabiashara Mkubwa wa Mjini Bariadi mkoani Simiyu,
Bw. Clement Mlanda Shigugulu ambaye anamiliki Hotel ya MS COMPLEX
amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka zawadi ya fedha
taslimu (kiasi ambacho hakikutajwa), kilo 50 za sukari, kilo 25 za unga
wa ngano na lita 40 za mafuta ya kula, ikiwa ni shukrani kwake kwa namna
uongozi wake ulivyochangia kuufungua mkoa wa Simiyu kiuchumi na kuwawezesha
wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara katika nyakati mbalimbali.
Amesema
kupitia uongozi wa Mhe. Mtaka kumekuwa na matukio makubwa yanayochangia
kuongezeka kwa mzunguko wa biashara mkoani Simiyu, ikiwemo Maonesho ya Kilimo
na Sherehe za wakulima Nanenane ambayo yamewaleta watu kutoka sehemu mbalimbali
hivyo kuwanufaiisha wafanyabiashara wa Simiyu hususani wamiliki wa hoteli na
nyumba za kulala wageni.
"
Jana nilienda Uwanja wa Nanenane nikakuta mambo mazuri, nilipokuja hotelini
kwetu nako nikakuta watu wamejaa, nikamuuliza baba(mume wake) kuwa tutampa nini
huyu Mkuu wa mkoa wetu kwa mambo mazuri anayotufanyia ya kutuletea
maendeleo hivi na kutuletea heshima mkoa wetu mpya wa Simiyu "
alisema.
"Nilimwambia
mume wangu nitampa zawadi yoyote kumshukuru ili moyo wangu ufurahi,
Nimemletea mafuta ndoo mbili za lita 20, sukari kilo 50,unga wa ngano
kilo 25, nampongeza sana na Mungu amzidishie aendelee na moyo huu wa kutuletea
maendeleo Mkoa wetu mpya wa Simiyu" alisisitiza Bibi. Elizabeth.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru
Mfanyabiashara huyo kwa zawadi hizo na akaeleza kuwa itakuwa ni kumbukumbu
katika maisha yake huku akifafanunua kuwa kazi anayoifanya ni wajibu wake
katika kuwaletea wananchi.
Ameongeza
kuwa mikoa mingi imekuwa kiuchumi kutokana mchango wa viongozi waliopo,
waliopita kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wafanyabiashara.
"Maendeleo
ndiyo nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kama ilivyokuwa kwa Marais, mawaziri
waliopita, na kwa mkoa wa Simiyu mchango wangu unaendeleza kile walichofanya
wakuu wenzangu wa mkoa walionitangulia, Marehemu Mabiti na baba yangu Elaston
Mbwilo"'alisema.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment