Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza akihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo)
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikagua miche ya maembe inayouzwa na mkulima Adam Warioba kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma alipotembelea Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akifurahi jambo na wananchi wa mkoa huo mara baada ya kikundi cha ngoma kutumbuiza katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Simiyu
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles
Tizeba amewapongeza wakulima, Wavuvi na wafugaji kote nchini kwa ufanisi wao
katika kazi kwani wameendelea kusaidia upatikanaji wa malighafi za viwanda
zinazohitajika huku akisisitiza kuwa sekta hizo ni muhimili muhimu katika
ustawi wa Taifa.
Alisema kuwa matarajio ya serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli ni kuhakikisha uwekezaji katika kilimo, ufugaji na uvuvi
unakuwa na tija kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia za kisasa na kuongeza
thamani ya mazao kwa kuzalisha bidhaa kupitia viwanda vidogo, vya kati na
vikubwa.
Waziri wa kilimo ameyasema hayo hayo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane
mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Alisema kuwa Uwekezaji katika sekta
hizo ukiimarishwa utasaidia kwenye matumizi ya teknolojia katika kuzalisha na
kuongeza thamani ya mazao kwa kuzalisha na kuongeza thamani ya mazao na hivyo
kuweza kuchangia zaidi katika kuongeza pato la Taifa, kuzalisha ajira na
maendeleo kwa ujumla.
Alisema kauli mbiu ya maonesho ya
nanenane Kitaifa mwaka 2018 inasema “Wekeza katika kilimo, Mifugo na Uvuvi
kwa maendeleo ya Viwanda” inahamasisha kuongeza uzalishaji wa tija ili
kuchangia ukuaji wa uchumi na kuifanya nchi iwe ya uchumi wa kati ifakapo mwaka
2025.
Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba amewapongeza
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Mara na Shinyanga kwa kujenga Jengo la Kudumu (Simiyu Exhibition
Hall), katika Uwanja wa Maonesho wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki na kushauri kanda
zote za Maonesho ya nanenane kuiga mfano kwa kanda hiyo, ili
wananchi waweze kupata elimu endelevu katika teknolojia za kilimo sambamba na
kutumika kwa Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa.
Alisema kuwa ni mategemeo yake kuwa katika eneo hilo
wakulima na wananchi kwa ujumla watapata uzoefu wa kilimo, hivyo kupanua wigo
na uelewa wa wakulima huku akiwashauri viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuona namna
kuhamasisha wafanyabiashara kujenga hoteli maeneo ya jirani na jengo hilo ili
kujiandaa na huduma kwa watu watakaokuwa wakifika kwa ajili ya maonesho hayo.
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa utaendelea kufanya maonesho
ya Teknolojia mbalimbali kila baada ya miezi mitatu katika Jengo
hilo, ili kuwapunguza kazi Watanzania kwenda nje ya nchi kushuhudia
maonesho hayo lakini pia kuvutia mataifa pengine kuja nchini kuonesha
teknolojia mbalimbali za kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment