Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua mashine ya mbalimbali za kilimo mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akijionea michoro mbalimbali ya ramani za nyumba mara baada ya kutembelea banda la VETA, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akimsikiliza Mhandisi wa Kanda ya Umwagiliaji Morogoro Mhandisi Senzia Maeda mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Umwagiliaji, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018.
Na
Mathias Canal, WK-Morogoro
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles
Tizeba Leo 6 Agosti 2018 amewaagiza waratibu wa maonesho ya nanenane
kuhakikisha Viuatilifu vinavyoonyeshwa kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima
Nanenane pasina kufuata utaratibu wa kisheria vinaondolewa haraka.
Waziri Tizeba ameyasema hayo
wakati akizungumza na wauzaji wa viuatilifu Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro
mara baada ya kutembelea banda la Tan Vaterinary ambalo linauza viuatilifu vya
aina mbalimbali zikiwemo dawa za virutubisho kwa ajili ya Nguruwe na kuku.
Alisema katika agizo hilo kuwa
viuatilifu vyote vinavyouzwa pasina nembo ya Mamlaka ya viwango Tanzania (TBS),
Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) na kampuni ya kutoa barcode za bidhaa
zilizofungashwa (GS 1) hazipaswi kuwepo kwenye maonesho ya Nanenane kote nchini
kwani kuruhusu viendelee kuuzwa ni hatari kwa wanyama sambamba na binadamu.
Alisema kuwa katika maeneo mengi
nchini udhibiti wa viuatilifu ni mdogo hivyo wakaguzi wa viuatilifu wanapaswa
kutilia mkazo ukaguzi ili kuzuia viuatilifu vinavyoingia nchini kinyume cha
sheria na taratibu za nchi.
Kuhusu elimu kwa wananchi juu ya
njia bora za kuhifadhi mahindi Waziri huyo anayeshughulikia sekta ya kilimo
nchini aliagiza elimu kutolewa kwa kina kwa wananchi ili wawe na uelewa mkubwa
pindi wanapomaliza kuvuna.
Alisema kuwa kumekuwa na
biashara ya vihenge jambo ambalo ni zuri lakini changamoto kubwa wananchi bado
hawajapatiwa elimu ya namna bora ya kuvitumia vihenge hivyo.
Aidha, amewataka washiriki
mbalimbali kutuma wawakilishi kwenye weledi kuhusu bidhaa wanazoonyesha kwani
kumekuwa na wawakilishi wengi ambao sio msaada kwa wakulima ambao wengi wao
wanatembelea katika maonesho hayo kwa mtazamo wa kujifunza.
Katika hatua nyingine akiwa
katika banda la maonesho ya Mifugo, Waziri Tizeba amewataka wataalamu hao wa
Mifugo kubadili mtazamo wa kifikra kwa kuonyesha bidhaa bora, "Kila mwaka
mnaleta Ng'ombe wa kisasa kwenye maonesho ya Nanenane wakati wanaokuja kujionea
maonesho wengi ni wafugaji wa Ng'ombe wa kienyeji, hivyo badilikeni leteni
Ng'ombe wa kienyeji" Alikaririwa Dkt Charles Tizeba
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment