METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 21, 2018

Wawekezaji nchini watakiwa kufuata nyayo za kampuni ya Kambas

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko pamoja na viongozi mbalimbali wilayani Songea, wakikagua eneo la uchimbaji madini ya Makaa ya Mawe katika machimbo ya Kambas wilayani humo.

Na George Binagi, BMG

Wawekezaji katika sekta ya madini nchini wametakiwa kuiga mfano wa kampuni ya “Kambas Group of Companies” inayochimba madini ya Makaa ya Mawe katika machimbo ya Kambas yaliyopo Kijiji cha Maniamba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko alitoa rai hiyo Julai 18, 2018 alipotembelea machimbo hayo na kufurahishwa na uwekezaji wa kampuni hiyo ya kizalendo na kushauri iongeze uwekezaji ili izalishe zaidi.

Mhe Biteko alieleza kufurahishwa na kampuni hiyo kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya madini na kulipa kodi serikali kuu pamoja na Halmashauri ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu imezalisha tani 5,138 na kulipa serikalini shilingi Milioni 16 ikiwa ni malipo ya mrabaha pamoja na ada ya ukaguzi huku pia ikilipa shilingi 1,000 katika serikali ya Kijiji cha Maniamba kwa kila tani moja ya Makaa ya Mawe inayouzwa.

Mwenyekiti wa kampuni ya "Kambas Group Of Companies" Yahya Kambaulaya alisema kwa sasa kampuni hiyo inazalisha tani 200 kwa siku huku matarajio yaliwa ni kuzalisha tani 600 hadi 700 kwa siku na kwamba hadi kufikia mwezi ujao matarajio yakiwa ni kuzalisha hadi tani 21,000 kwa mwezi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Ruvuma Mhe Chritina Mndeme alitoa rai kwa kampuni ya Kambas kuongeza uzalishaji zaidi huku ikipanua soko lake ili kuuza Makaa ya Mawe hadi nchi jirani ya Msumbiji huku akiipongeza kwa mikakati yake ya kuanza uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe.
Mwenyekiti wa kampuni ya "Kambas Group Of Companies" Yahya Kambaulaya (kushoto) inayochimba Makaa ya Mawe kwenye machimbo ya Kambas wilayani Songea akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko (kulia) alipotembelea machimbo hayo Julai 18, 2018
Mkuu wa Wilaya Songea mkoani Ruvuma Mhe.Pololet Mgema (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko (wa pili kushoto) alipotembelea machimbo ya Kambas wilayani humo
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko akizungumza baada ya kufanya ziara kwenye machimbo ya Kambas wilayani Songea
Mkuu wa Mkoa Ruvuma Mhe.Christina Mndeme akizungumza jambo baada ya Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko kufanya ziara kwenye machimbo ya Kambas
Mkuu wa Wilaya Songea Mhe.Pololet Mgema (kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko ya kutembelea machimbo ya Kambasi wilayani humo
Mwenyekiti wa kampuni ya "Kambas Group Of Companies" Yahya Kambaulaya (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko alipotembelea machimbo ya Kambas wilayani SOngea
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa Ruvuma Mhe.Christina Mndeme (kushoto), Mkuu wa Wilaya Songea Mhe.Pololet Mgema pamoja na viongozi wa kampuni ya Kambas Group of Companies wakijionea eneo la kuuzia makaa ya mawe (Bandari Kavu) iliyopo Kijiji cha Likuyu Fusi wilayani Songea
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com