Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman
Jafo wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu
zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa
kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa
mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa
taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato
cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
1. Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo
akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi
la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na
kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya
wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana
31,884 na wavulana 39,020
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini
kwake leo, Mhe. Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu
kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga
na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.
Mhe. Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa
wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za
Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya
Sanaa na biashara.
Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na
vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya
Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI)
na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
Mhe. Jafo alisema jumla ya wanafunzi
11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya
awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa
na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Aliagiza wanafunzi wote waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2018 wahakikishe wanaripoti katika shule
zao kuanzia tarehe 15,Julai,2018 na
atakayechelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya
kuripoti nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Mhe. Jafo alisistiza kuwa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato
cha Tano na Vyuo vya ufundi umefanyika
kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule, hakutakuwa na fursa ya
kufanya mabadiliko yeyoye ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi kwenye shule
husika.
Alisema wanafunzi waliopangwa kwenye vyuo
vya kati wanapaswa kudhibitisha kukubali kujiunga na kozi walizochaguliwa hadi ifikapo 8 Agosti, 2018 ili kuthibitisha kuwa wamekubali kozi na vyuo walivyopangiwa
kwa wanafunzi watakaoshindwa kuthibitisha nafasi yake itachukuliwa na
mwanafunzi mwingine.
Amewapongeza walimu, wazazi na wakezi kwa
juhudi walizozifanya katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi kufaulu vizuri
na kuwaagiza kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto nchini.
Aidha ametoa wito kwa Wakuuwa Mikoa, Wakuu
wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha
azima ya Serikali ya kila Tarafa kuwa na shule ya Kidato cha Tano inatekelezwa
ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu
Kidato cha Nne kuapata na fasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha 5 na 6.
“Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote
za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi gharama za usafiri kwenda
shule za mbali nje ya Mkoa” Alisema Jafo
Aidha amesema kutokana na ongezeko la
ufaulu wa masomo ya Sayansi kila shule zinazoanzishwa kuhakikisha zinajengwa
maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa tahasusi za Sayansia ambao ufaulu
wao umekuwa ukiimarika kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment