METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 11, 2018

“PAMBA ISITOKE KIJIJINI KABLA MKULIMA KULIPWA FEDHA ZAKE” DKT TIZEBA

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora, Picha Zote Na Mathias Canal, WK. Leo 11 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akishuhudia zoezi la uuzaji na ununuzi wa pamba katika kijiji cha Ishihimulua kilichopo Kata ya Bukumbi Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Wakazi wa kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji na kata ya Miguwa Wilayani Nzega akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.

Na Mathias Canal, WK-Tabora

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amepiga marufuku kwa wanunuzi wa pamba kuondosha pamba ya wakulima kwa maelewano ya kulipa baada ya siku kadhaa badala yake ameagiza wakulima wa pamba kulipwa fedha zao kabla ya pamba kusafirishwa.

Dkt Tizeba amepiga marufuku hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Tabora leo 11 Juni 2018 wakati akihutubia wakulima wa pamba katika kijiji cha Mulidede na Ishihimulua vilivyopo katika Wilaya ya Uyui sambamba na kijiji cha Miguwa kilichopo katika Wilaya ya Nzega.

Dkt Tizeba alisema kuwa kumekuwa na ombwe la wakulima kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka pamba kwenye kampuni za ununuzi jambo ambalo linachelewesha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wakulima hao na familia zao kwa ujumla kwa wakati tarajiwa.

Alisisitiza kuwa ili pamba iweze kusafirishwa kwenda popote baada ya mauziano ni lazima mkulimwa alipwe stahiki zake kwa wakati sio kuishi kwa kukopesha bidhaa hiyo muhimu isiyokuwa na uduni wa soko.

Dkt Tizeba amemaliza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea mkoa wa Singida ambapo pamoja na mambo mengine anakutana na wakulima na wanunuzi wa pamba ili kujionea zoezi la ununuzi na uuzaji wa pamba.

“Lakini ndugu zangu wakulima na ninyi ni lazima niwaambie ukweli baada ya kuuza pamba mnapaswa kuwa makini katika matumizi ya fedha zenu kwani endapo mkitumia hovyo vile vile fedha hizo zitamalizika pasina kufanya jambo la maendeleo kwa familia na jamii kwa ujumla” Alikaririwa Dkt Tizeba

Katika hatua nyingine Dkt Tizeba ametangaza neema kwa wakulima wa pamba kwa kuwafahamisha kuwa kila mwananchi aliyelima pamba ni mwanachama wa chama cha ushirika AMKOS hivyo ana sifa za kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ushirika.

Tayari waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba amewasili Wilayani Kahama ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa masoko ya Tumbaku Kitaifa hafla itakayofanyika katika mkoa wa kitumbaku-Kahama 12 Juni 2018.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com