Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa
wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni
za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi
akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Mufindi wakimusikiliza kwa umakini mkubwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila wakati wa ziara yake ya kwanza ya kikazi
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Iringa wakiwa kazini kupata habari kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akipokelewa na green gard wa wilaya ya Mufindi na kupewa heshima anayostahili
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akivishwa skafu nagreen gard wa wilaya ya Mufindi
NA FREDY
MGUNDA,IRINGA.
MWENYEKITI wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa
wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni
za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi
akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.
Akizungumza na wajumbe
wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo mjini Mafinga,Chalamila alisema kuwa
amesikia kuwa kuna wanachama wameanza kupita pita kuanza kufanya kampeni za chini
chini na kusababisha wapunge wa majimbo hayo kutofanya kazi zao kwa ufanisi.
Chalamila
aliyataja Majimbo ambayo wananchama hao hao wameanza kupita ni jimbo Mafinga
Mji linaloongozwa na Mbunge Cosato Chumi, jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamudu
Mgimwa na Mufindi Kusini Meldrad Kigolla.
Alisema kuwa anafanyakazi
kwa ukaribu na vyombo ya usalama wa taifa ili kupata taarifa ambazo ni sahihi na
kuwabaini baadhi ya wana CCM walioanza kujitengenezea mazingira kwa ajili ya
kupata uteuzi katika uchaguzi mkuu ujao kinyume na kanuni hizo za chama.
Chalamila aliwataka viongozi
waliochaguliwa na wananchi kufanya kazi kwa kujituma na kukitendea haki chama
cha mapinduzi (CCM) ili kiendelee kuaminiwa na wananchi
Aidha Chalamila
alisema katika mazingira ya kusikitisha alisema wana CCM wengine wanaoshiriki
kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa
wajumbe wa vikao vikubwa vya chama na katika onyo lake kwao aliwatahadharisha
dhidi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwao.
“Waacheni wabunge
na madiwani waliopo wafanye kazi, wamalize miaka yao mitano kwa uhuru.
Mliwachagua wenyewe, wapeni nafasi na kama mnataka kuamua vinginevyo subirini
hadi pazia la uchaguzi litakapofunguliwa lakini sio sasa,” alisema Chalamila.
Mwenyekiti huyo
aliwataka wajumbe hao,kuhakikisha wanaweka mikakati ya
ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa
kuhakikisha wanazirudisha ndani ya ccm kata 2
zilizochukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani humo.
Chalamila
alizungumzia visasi na mioyo ya kinyongo miongoni mwa wana CCM wakati na baada
ya chaguzi za chama na jumuiya zake, na za serikali akisema; mambo hayo
yamekuwa yakisabisha mpasuko wa muda mrefu ndani ya chama hivyo ni lazima
yaachwe.
“Visasi na
vinyongo vimevuka mipaka. Wapo pia wana CCM ambao kila kukicha kazi yao ni
kuwazushia na kuwachafua wenzao kwamba ni wafuasi wa vyama vingine vya siasa
kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba wana mienendo
mibaya ndani ya chama mambo ambayo si ya kweli. Wana CCM tupendane na
tutendeane mema,”alisema Chalamila.
Aliwataka wenye
taarifa za wanachama wenye mienendo mibaya na inayotishia uhai wa chama
waziwasilishe kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama ili ziweze
kufanyiwa kazi.
Mwenyekiti Chalamila
alimalizia kwa kusema kuwa watawanyang’anya kadi wanachama wote ambao watakuwa
wanaendelea kuvunja kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi
“Kwakweli nitakuwa
mkali sana na nitasimamia vilivyo kwa wale ambao watakuwa wanavunja
kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuwa madaraka hayo ninayo
kwa mujibu wa kanuni na sheria za chama chetu” alisema Chalamila
Baada ya kukutana na
halmashauri kuu ya CCM ya wilaya ya Mufindi, Chalamila anatarajiwa pia kukutana
na na wajumbe wa vikao hivyo wa wilaya ya Kilolo, Iringa Vijijini na Manispaa
ya Iringa katika ziara yake anayofanya akiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele
0 comments:
Post a Comment