Baadhi ya wananchi wa kata ya Malambo Mjini Bariadi , waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Malambo Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu, inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi takribani 1000 wa Kata ya Malambo wilayani Bariadi
wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Festo Kiswaga wamejitokeza kwa wingi
kuchimba msingi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mkoa
wa Simiyu ambayo inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu .
Wakizungumza katika nyakati tofauti baadhi ya wananachi
walioshiriki katika zoezi hilo wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka kwa maono yake katika kuleta maendeleo ya elimu mkoani humo na kuahidi
kuwa watahakikisha wanamuunga mkono ili malengo ya kuwa na shule ya vipaji
maalum yanatimia.
“Tunamshukuru Mkuu wetu wa Mkoa kwa kuja na maono haya ya kuwa
na shule ya Ufundi ya Mkoa na sisi kama wananchi wa eneo
hili tunamuunga mkono kiongozi wetu, nitoe wito kwa wananchi
wenzangu kila mmoja aweze kuchangia alicho na uwezo nacho ili tuweze
kujenga shule yetu hii ikamilike na watoto wetu waanze kusoma” alisema
Christina Matulanya Mkazi Malambo Bariadi.
Diwani wa Kata ya Malambo Mhe.Kitebo Kitebo amesema wananchi wa
Kata ya Malambo kwa pamoja wameonesha ushirikiano toka walipotangaziwa kwa mara
ya kwanza juu ya kuanza kwa ujenzi wa shule hiyo, hivyo akawaomba kuendelea
kushirikiana mpaka shule hiyo ikamilike.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amewashukuru
wananchi wake na akawaomba waendelee kuonesha ushirikiano katika kufanikisha
ujenzi wa shule hiyo ili wawe mfano bora kwa wilaya nyingine zitakapoanza
kujenga shule za vipaji maalumu pia.
Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi Wilaya ya Bariadi Nicholaus Kasendamila amesema Jitihada hizo za
Ujenzi wa Shule hiyo ya Mkoa zilizoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu lazima ziungwe Mkono ambapo amewataka Wananchi kuweka pembeni
siasa kwenye suala hilo la Maendeleo
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ambaye aliwatembelea Wananchi hao
amesema Kuwepo kwa Shule hiyo ya Ufundi kutaleta chachu kubwa katika
kuwapata watalaam wa fani mbalimbali katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya
awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda na akawataka wazazi kuwasisitiza watoto
wao kusoma kwa bidii.
“Mkoa wa Simiyu
unajipambanua kama Mkoa wa viwanda ni lazima tuwe na shule ambazo watoto wetu
kwenye mitaala yao wanapomaliza kidato cha nne wanakuwa na stadi za ufundi za
kujiendeleza kimaisha, tunataka tujenge shule yenye karakana nzuri za ufundi
watoto watakaopita hapa waweze kuendesha maisha yao, tunataka shule hii ijibu
mahitaji ya mkoa” alisema
Aidha, Mtaka amesema
hadi sasa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia shule hiyo na mpaka sasa
jumla ya shilingi milioni 157 zimetolewa na wadau hao ili kuunga mkono ujenzi
wa shule hiyo na Serikali imetenga jumla shilingi milioni 58 kwa ajili ya
ujenzi wa Jengo la Utawala.
Ameongeza kuwa baada
ya kukamilisha shule hiyo ya Ufundi, Mkoa huo unatarajia kujenga shule ya
Wasichana , Shule ya Wavulana na shule maalumu ya mchepuo wa Kilimo ambayo
itatumika kama sehemu ya mazoezi kwa vitendo kwa Chuo cha Kilimo Sokoine(SUA).
MWISHO
0 comments:
Post a Comment