METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 23, 2018

RITTA KABATI CHALLENGE CUP MSIMU 2018 WAFUNGULIWA RASMI,TIMU ZAOMBWA KUCHUA FOMU KUSHIRIKI

 kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo  vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani Iringa mapema hii leo

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Kamati ya ya mshindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha radio cha Nuru Fm.

“Naomba viongozi wa vilabu vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya nambari 0714201006  au mnipigie mimi mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela

Malekela alisema kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani Iringa,Kuonesha uwezo wa vijana na kutengeneza ajira  kwao,Kujenga kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi,Kutoa burudani kwa wakazi wa iringa kwa  mchezo wa mpira wa miguu,Kuwakutanisha vijana pamoja ili kuzungumza lugha moja ya kimichezo na maendeleo,Kuwaepusha vijana na makundi au vijiwe visivyo faa na Kuhamasisha michezo katika mkoa wa Iringa,kutimiza agizo la makamu wa raisi juu ya kufanya mazoezi

“Sasa hapo utagundua kuwa jinsi gani mashindano hayo yalivyo yanaumuhimu katika kukuza vipaji hapa mkoani kwa ustawi wa soka letu la nchi hiii” alisema Malekela

Aidha Malekela  alizitaja zawadi pamoja na vifaaa ambavyo vitatolewa kwa timu shiriki


VIFAA
 msimu wa mwaka huu wa 2018 Kupitia mdhamini RITTA KABATI tunataraji kutoa vifaa  vya michezo kama ifuatavyo kwa timu shiriki.
Kifaa
Muhusika
idadi
Mipira ya mazoezi
Timu shiriki
Mpira mmoja (1)
Jezi za mechi
Timu shiriki
Jezi set 1
Jezi za waamuzi
Waamuzi
Set 6


D: ZAWADI.
No.
Muhusika
Zawadi ya kwanza
Zawadi ya pili
1.   
Mshindi wa kwanza
Kombe  1,000,000.00
2,000,000.00
2.  
Mshindi wa pili

1,000,000.00
3.  
Mshindi wa tatu

500,000.00
4. 
Mchezaji bora

100,000.00
5.  
Mfungaji bora

100,000.00
6. 
Golikipa bora

100,000.00
7.   
Waamuzi bora

100,000.00
8. 
Kikundi bora cha ushangiliaji

200,000.00
9. 
Timu yenye nidhamu

100,000.00

Jumla
1, 000,000.00
4,200,000

Ligi yetu itakuwa kama msimu uliopita  tutakuwa na hatua ya mtoano kulingana na timu zitakazo jitokeza kuchukua fomu za kushiriki mashindano haya na hatimaye kupata timu kumi ambazo zitacheza hatua ya makundi mawili na kupata timu nne ambazo zitacheza nusu fainali na hatimaye fainal

Matarajio yetu mashindano yatazinduliwa rasmi tarehe 10 mei 2018 siku ya jumapili wapi na itakuwaje na nani atakuwa mgeni rasmi hayo yote yatawekwa bayana muda si mrefu.

Kama kamati tunamshuru sana Mh. Mbunge Ritta Kabati kwa kukubali kudhamini mashindano haya na kuwathamini vijana wa mkoa wa iringa fedha hii ambayo anaitoa kwaajili ya kufanya yote haya angeitumia kwa kazi zake nyingine kwa maendeleo ya familia yake lakini kwa kutambua nafasi aliyonayo na kuwathamini vijana ndio maana anafanya haya yote hivyo sisi kamati tunamshukuru na kumpongeza aendelee kuwa na moyo huu.

Leo tarehe 21 / 5/ 2018  ndio  rasmi dirisha la uchukuaji fomu za usajili linafunguliwa na litafungwa  tarehe 31 /5/2018 – gharama ya fomu ya usajili wa timu kwenye mashindano haya ya RITTA KABATI CHALLENGE CUP IRINGA 2018 ni  shilingi 30,000.00 tu na fomu zinapatikana kwa kamati ya mashindano na si kuingine,  unaweza kupiga namba hii kwa maelezo 0715779233 AU 0714201006 AU 0762687732, au wanaweza wakafika nuru fm ndiko viongozi tulipo.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com