METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 11, 2018

Mkuu wa Mkoa Simiyu alishukuru shirika la Amref kwa kubabidhi "Ambulance"

Na Binagi Media Group

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.Antony Mtaka amelishukuru na kulipongeza shirika la Amref Health Africa kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha huduma za afya katika mkoa huo.

Mhe.Mtaka ametoa pongezi hizo leo Mei 11, 2018 wakati akipokea gari la wagonjwa (Ambulance) lililotolewa na shirika la Amref kwa ajili ya hospitali teule ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa gari hilo.

Mhe.Mtaka amesema shirika hilo kupitia mradi wake wa Uzazi Uzima limesaidia kuboresha huduma mbalimbali za afya mkoani Simiyu ikiwemo ujenzi na ukarabati Zahanati, Vituo vya Afya, wodi (Mama Ngojea) pamoja na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.

Meneja Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr.Serafina Mkuwa amesema gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na kodi na kwamba limekabidhiwa kupitia mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.

Shirika la Amref Health Africa linatekeleza miradi mbalimbai ya afya hapa nchini kupitia ufadhili ya serikali ya Canada.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com