Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe *Kisare Makori* ametoa maagizo matatu kwa Uongozi wa Kiwanda cha "Royal Soap Detergent" kilichoko eneo la External Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Ametoa Maagizo hayo leo alipozuru katika Kiwanda hicho akiwa ameambatana na timu zima ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ubungo baada ya kupata taarifa za malalamiko ya athari za mazingira zinazotokana na shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Kwanza ameutaka uongozi wa kiwanda cha "Royal Soap Detergent" kufanya kazi kwa kuzingatia masharti ,matakwa ya uzalishaji, weledi,usalama na usafi katika shughuli za uzalishaji ndani ya kiwanda hicho.
Pili uongozi wa wilaya utaleta wataalamu kwa kushirikiana taasisi zingine za serikali kufanya ukaguzi wa vifaa na mitambo katika kiwanda hicho kama ni salama kwa afya za wananchi katika eneo hilo na hata kwa wafanyakazi.
Tatu Uongozi wa kiwanda uangalie uwezekano wa kulipa fidia kwa wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho kwa wale ambao watakuwa tayari kuhama eneo hilo.
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema kwa wale ambao waliathirika na uchafu wa kiwanda hicho wakaugua na kulazwa hospitali tutakaa na kuangalia sheria zikoje tuone namna ya kuwapa fidia, niwasihi muendelea kuwa na subira tutarudi tena kuwaeleza utekelezaji wa maagizo hayo.
Maagizo hayo ya Mkuu wa Wilaya Mhe *Kisare Makori* kwa kiwanda hicho cha "Royal Soap & Detergent "yametolewa kutokana na malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na Kiwanda hicho kuathiriwa na uchafu wenye kemikali ambazo zinahatarisha afya za wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment