METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 4, 2021

RAS SINGIDA AUPIGA MWINGI , RPC AONDOKA NA KUKU KWENYE BONANZA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU KIMKOA , NI RAHA TUPU!

 












Na Hamis Hussein - Singida

Mkoa wa singida unaungana na mikoa mingine nchini katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania. kuelekea katika maadhimisho hayo  mkoa wa singida umeaanda matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na bonanza la ufunguzi , kutembelea hospitali kufanya usafi na shughuli zingine .

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko  Desemba 4, 2021 amefungua rasmi  maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru Tanzania Bara yaliyofanyika ki Mkoa wilayani Manyoni mkoani Singida katika uwanja wa Jumbe ambapo Watumishi mbalimbali walishirikishwa.

Katika hotuba yake kwa Watumishi kutoka wilaya ya Ikungi, Manyoni, Iramba, Singida mjini, Mkalama na Itigi RAS amewashukuru Watumishi hao kwa nidhamu kubwa walionesha wakati wa bonanza la michezo lililofanyika katika uwanja huo na kushirikisha michezo ya kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume, netiboli, mpira wa miguu, kukimbiza kuku, mcho wa bao, riadha na mashindano ya kula.

Hata hivyo RAS Mwaluko akatumia fursa hiyo  kuzipongeza timu mbalimbali zilizoshinda katika bonanza hilo pamoja na watumishi walioshiriki katika michezo na mazoezi mbalimbali ambapo akawaasa kuendelea kufanya mazoezi hata baada ya bonanza kwisha ili kulinda afya zao.

Mwiongoni mwa walioshinda katika bonanza hilo ni kamanda wa polisi mkoa wa singida ASP stella Mutabihirwa alijishindia mchezo wa kufukuza kuku akiwashinda , meya wa manispaa ya singida Yagi Kyaratu , na RAS mwenyewe.

RAS  Singida akawataka watumishi hao kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru kwa kujitathimini  walipotoka walipo na wanapokwenda ili kuona maendeleo ambayo nchi yetu imeweza kuyafikia katika kipindi hicho. 

Wadau wengine walioshiriki maadhimisho hayo ni pamoja na Henry Kapera  ambaye ni  Afisa michezo wa Mkoa wa Singida ak akaeleza umuhimu wa michezo  kwa watumishi kuwajenga watumishi  hao ki afya.

Kapera akamalizi kwa kusema  mkoa  huo una mkakati kabambe kuendeleza michezo hiyo pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.




Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com